KOMBE LA DUNIA LIMEFIKA PATAMU,NJE AMA NDANI

MTOANO-1

Kombe la dunia limefika hatua ya nje ndani yaani kubaki ama kuondoka ndani ya michuano hii nchini Urusi.


Katika hatua hii ya wiki hii timu mbili katika timu nne zilizoko makundini zitafuzu wakati timu nyingine zitafuzu hatua inayofuata timu nyingine zitaaga mashindano,nyingine zishafuzu huku nyingine zinasubiria maajabu ya Mussa.

Kundi A na B zinacheza leo huku timu 2 za kundi A zilizofuzu zinajulikana na kundi B timu tatu zina nafasi ya kufunzu lakini 2 tu ndo zitaendelea.

Kundi A timu zilizofuzu ni Urusi na Uruguayi lakini zitacheza mchezo ambapo mshindi atakuwa kiongozi au mshindi wa kundi mwingine atakuwa msindikizaji wa kundi wote wataenda raundi ya 16 bora.Nchi za Saudia na Misri watacheza nani atakuwa mshindi wa tatu ama mfunga mlango wa kundi.

Kundi B nao watapigana vikumbo lakini utamu wa siku unakuwa hapa sasa timu tatu zinaweza kufuzu lakini timu moja tu ndo habari ni mbaya.Timu ya Uhispania itafuzu kama ikipata droo na Morroco ama Ureno akiifunga Iran ama afugwe magoli mengi na Morroco na mechi ya Ureno afugwe magoli machache na Iran. 


Kwa upande wa Ureno droo na ushindi utampeleka raundi ijayo.lakini ushindi wa Iran utampa nafasi Iran kwenda raundi ijayo.

Morroco ana nafasi hana kamilisha ratiba.

Kombe la  dunia na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe: barthaprosper@gmail.com




Maoni