KOCHA WA UINGEREZA KAKIRI UKWELI KWA BRAZILI NA UJERUMANI

Uingereza itakuwa timu ya tatu yenye wachezaji wenye umri mdogo kwa wastani wa timu zitakazocheza kombe la Dunia ilihali kocha wao Gareth Southgate anatambua kuwa kikosi chao si kikali kama timu nyingine kwenye mashindano.

Tengia Southgate aanze kukinoa kikosi hicho Septemba mwaka 2016 kumekuwa na mabadiliko makubwa sana ya kustaajibisha katika soka la timu hiyo ya taifa yenye miaka zaidi ya 50 bila kombe.

"kati ya Panama na Tunisia hatuwajui sana kama tunavyowajua Ubeligiji lakini watakuja na moyo mkubwa na watakuwa na matumaini madogo sana na itawafanya kuwa hatari" Akizungumzia kundi aliloliangukia katika kombe la Dunia.

"inategemea ndoto yako,nafikiri tunajua tulipo.....kuwa wa 12 duniani tunajihusisha,lakini hatuko bora kama Ujerumani na Brazili.tuna wachezaji wadogo ni mda kwao kuwasukuma mbele tuko katikati ni mda pia wa kuwatumia hawa  vijana baadaye tuanze kutwaa mataji" kuhusu ndoto yake kuhusu kikosi hiki.

"Goli langu ni kushangaza watu,kabisa na i shaanza kuonekana na nafikiri ni vizuri" akiongezea kama timu yake inaweza kushangaza dunia.

"Hatujasahau kabisa ,ukizika kitu na ujiulizi kwa nini nafikiri utakuwa ujapata somo,ilikuwa mbaya sana,lakini wachezaji wamekuwa wawazi,tumetumia njia ya kuwapa moyo na nzuri kuweka utimamu wao vizuri" Gareth Southgate akifunguka kuhusu kutupwa nje euro 2016 na Iceland.

"Tumecheza dhidi ya Ujerumani na Brazili kwa miezi ya hivi karibuni na wote wako vizuri,Hispania wanajiunga na wako vizuri Ubeligiji nao wako vizuri sana,naweza sema Brazili wana nguvu,njia na ujuzi wa kwenda kushinda" Alipoongezea kuhusu timu zenye nguvu.

Kombe la Dunia na Prosper Barthalomew.

Maoni