FIFA WAWAJIBU BRAZILI NA BARUA YAO

Chama cha soka cha Brazili waliandika barua kwa shirikisho la soka la dunia FIFA wakidai baadhi ya matukio kufanyiwa wakati kulikuwa na uwezo wa VAR kurudia matukio hayo katika mchezo wao dhidi ya Uswinzi,lakini shirikisho limetupilia mbali malalamiko hayo.


FIFA waliwaandikia hawa mabigwa mara tano wa kombe la  dunia kuwa VAR ilitumika vyema katika mechi yao dhidi ya Uswinsi uwanjani Rostov-on-Don na hawaoni makosa wanayoyadai katika mchezo huo.

Huku FIFA wakisema matukio yote yalirudiwa katika chumba cha  VAR lakini Shirikisho limekataa kutoa audio yoyote kutoka katika chumba hicho.

Na huku Shirikisho likidai limefurahishwa na matumizi ya VAR mpaka sasa nchini Urusi.


Huku wakisema kutakuwa na maoni mengi,lakini hawawezi dili na tukio moja moja katika maoni ya watu kuhusu mfumo wa VAR.

Kombe la dunia Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.

Barua pepe:barthaprosper@gmail.com

Maoni