DIEGO MARADONA KACHANGANYIKIWA NA ARGENTINA

Diego Maradona aliwaaishwa hospitalini baada ya kupata huduma ya kwanza baada ya mchezo wa Argentina dhidi ya Nigeria kuisha kwa Argentina kupata ushindi wa kimuujiza.


Mshambuliaji huyo wa zamani na mshindi huyo wa kombe la dunia 1986 alikuwa anaangalia mechi kuanzia jukwaani uwanjani St Petersburg amekuwa akisafiri na Argentina kwa muda sasa katika mechi zote tatu amezihudhuria huku timu hizo zikikosa matokeo mpaka jana walipopata ushindi muhimu katika soka lao.

Video ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha Maradona anasaidiwa kutembea kutoka alipokuwa anakaa mpaka vyumba vya jukwaa kabda ajapelekwa hospitalini.

Gazeti la kiargentina linadai ya kuwa alikuwa amekubwa na (pressure blood) na alitibiwa na kuondoka baada ya kupata huduma ya kwanza.

Mshambuliaji wa zamani wa England na mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 1986 Garry leneker amesema staa huyo wa miaka 57 alikuwa hatarini kupata ugonjwa wa stroke baada ya kuonesha vidole vya kati baada ta goli la Maros Rojo.


Argentina itacheza dhidi ya Ufaransa jumamosi katika raundi ya 16 bora huku jana magoli yao yakifugwa na Lionel Messi na Marcos Rojo huku la Nigeria likifugwa na Victor Moses.


Kombe la  dunia na Prosper Bartholomew.

Simu:+255716243875.



Maoni