klabu ya Bayern Munich imeweka bei rasmi kwa kiungo wake mhispaniola Thiago Alcantara ambaye amekuwa windo kuu la klabu ya Barcelona baada ya Antonie Graizemann kuamua kusalia klabuni Atletico Madrid.
Barcelona wamefanya kumuulizia mchezaji huyo huko Bavarian na kuambiwa huduma yake itapatikana kama wataweza kufikia kitita cha euro 70 milioni kuanza mazungumzo ya kiungo huyo mhispaniola.
Thiago aliichezea klabu ya Barcelona kabda ya kushidwa kuzoea maisha ya klabu hiyo na kupigwa bei klabuni Bayern na pia kuna uwezekano Digne akaingizwa katika mazungumzo kwani mabigwa hao wa ujerumani wanaisaka saini yake.
Habari na Prosper Bartholomew.
Maoni