Tengia Iniesta afanye uamuzi wa kwenda kujiunga na klabu ya Vissel Kobe Wacatalunia wakaanza kumnyatia kama mtu sahihi wa kuziba pengo la mkogwe huyo ambaye alijitolea kila kitu kwa klabu hiyo.
Tatizo ni moja kwa klabu hii ya Barcelona ni bei ambayo klabu ya Juventus itaitaja kama mauzo ya kiungo huyu mchezeshaji , mabigwa hawa wa Serie A hawatamuuza mchezaji huyu wa zamani wa Roma chini ya euro milioni 80.
kama Barcelona watafeli kumtwaa kiungo huyu hawana budi kurudi katika ardhi ya Brazili na katika klabu ya Gremio iliyocheza fainali ya kombe la dunia kwa ngazi ya klabu na kupigwa na Real Madrid bao 1 kwa bila mwezi decemba mwaka jana na kumchukua kiungo wao Arthur Melo.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni