Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Real Madrid Marco Asensio amekiri ya kuwa kuna tamanio la usajili kutoka katika klabu ya Liverpool lakini hafikiri saivi katika suala la usajili kwa muda huu.
Majogoo wa Anfield baada ya kupoteza dhidi ya los blancos katika fainali ya ligi ya mabigwa ulaya wana mpango wa kuimarisha kikosi chao licha ya kusajili majembe kama Fabinho na Naby Keita wana itaji kumsajili pia winga huyu ambaye bado ni kinda licha ya kufeli kumtwaa Fekir kutoka Lyon.
Licha ya Liverpool kutoa tamanio lao,Asensio amekiri masuala ya usajili yataongelewa baada kombe la dunia kufika tamati.
"Tamanio la Liverpool limekuja,lakini limeondoka mimi niko kwa ajili ya timu ya taifa saivi" Asensio akikiri.
"Mwishoni tutaongelea,saivi kichwa changu kiko kinafikiria kuhusu hapa Urusi" Asensio aliongezea.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni