2010 Argentina ilikua na kikosi kamilifu na hamna mtu ambae angeweza kuibeza kwa kuangalia majina tuh yawachezaji timu ilikua inatisha na wapinzani wake walikua wanaichukulia vyema kabla hawajakutana nao. Kikosi Hicho kilikua chini ya nahonda Javier Mascherano,Carlos Tevez , wakiwemo nyota kama Lionel Messi na Diego Millito, pia katika benchi walikuepo vijana wa kazi kama Pastore na wengine wengi. Lakini walishangaza Dunia baada ya kuwa na uchache wa mabao, na hata team ya taifa ya Nigeria mbayo ilikutana nao katika mchezo wa kundi B, walihangaika sana kuifunga. Safari ya Argentina ilikua ya kawaida sana na kushindwa kufanya makubwa katika kombe hilo.
Zikapita siku, miezi, mwaka, na miaka 4 ikakamilika tukakutana Brazili. Sasa hivi Argentina ilikua ina kikosi kizuri sana, Kikosi ambacho kilikua na vijana na pia wachezaji kama wote walikua muhimu katika klabu walizotoka. Mashabiki wa soka ulimwenguni walikiangalia kikosi hicho na wengi hawakuogopa kukiwekea kete kwamba mwaka huu, argentina ndoo ni yake. Pila kuchimba sana kikoso hicho kilichokua kikinolewa na Alejandro Sabella kilikua cha kujiaminisha na hata Raisi wa Argentina alikua anasubilia tarehe ya fainali ili apokee kombe hilo ikulu. Ikumbukwe mwaka huo Lionel Messi ambae ndo nahodha wa timu hio alikua ameshachukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia *ballorn d'or* mara tatu (2010,2011,2012) kikosi kiliundwa na nyota kama, Gonzalo Higuain, Angel Di Maria, Marcos Rojo, Sergio Aguero na wengine wengi ambao kipindi hicho walikua katika ubora wao. Hamna mtu ambae angeweza kukataa kwamba argentina sio tishio, kiufupi argentina alikua GOLIATHI. Na kiukwel alifanikiwa kufika fainali dhidi ya wazee wa kazi ujerumani.
(TANGAZO)
"TUNATANGAZA MATANGAZO YOTE PICHA ,YA VIDEO ISIYOZIDI DAKIKA MOJA NA NUSU,NA MANENO PIA KWA BEI RAHISI SANA HASA KIPINDI HIKI CHA KOMBE LA DUNIA SIKU MARA TATU NA BONUSI YA KUTANGAZWA KWA SOCIAL MEDIA ZETU ZOTE WASILIANA NASI KUPITIA 0716243875"
Hawakutenda haki kabisa ndani ya dakika tisini za mchezo, higuain huyo alikua sijui ni wa wapi anii sio yule tunaemjua siku zote. Messi ambae dunia nzima ilikua inammulika lakini hakufanya lolote kuisaidia taifa lake, ambalo kweny mechi hio ililala kwa goli moja lililofungwa na mtoto mdogo tuh Mario Gotze. Ikawa ndo basi tena Goliathi akaanguka kwa jiwe moja tuu la Daudi.
Mwaka huu, 2018 mashabiki wa Argentina bado wana moyo na timu yao licha ya kuchapwa Bao 6 na mpinzani wao Hispania. Lakini Bado kikosi hicho hakionekani kama ni dhaifu pamoja na lawama za mashabiki kwamba kwenye kikosi chao hajajumuishwa Mauro Icardi ambae kamaliza ligi kuu italia na zaidi ya bao 20. Na kocha wa Argentina ameita safu ile ile ya ushambuliaji ambayo ilifeli mwaka 2014, Higuain , aguero, Messi. Timu yenyewe ina imani, wachezaji wote wana imani, ila mashabiki imani yao ni haba. Kwa sababu katika miaka sita iliyopita argentina kacheza Fainali 4, na amefungwa zote. Kocha wa Argentina ametoka ofisini na ticket za kwenda Russia akiahidi kwamba Lazima achukue kombe kwa sababu kama kufika fainali wamefika sana, ila Hawana ndoo kabatini na watu wamechoshwa na wimbi hilo la nuksi, wengine wanasema messi ndo nuksi labda mpaka astaafu ndo watachukua ubingwa. Na kama mwaka huu Goliathi ataonewa tena kama ilivyokila mwaka, basi argentina itabidi waanze kutafuta mchawi wao nani, kwa sababu kikosi wanacho, kocha wanae, wachezaji bora wanae,
KWANINI WASHINDWE
Kombe La Dunia na Rugambwa (infantino)
Simu :0629546461
Maoni