Klabu ya Chelsea inamilikiwa na bilionea Mrusi Roman Abrahimovic.
Aliinunua klabu hiyo mwaka 2003 ambapo kumekuwa na mabadiliko ya hali ya juu ikiwemo kutwaa mataji mengi kwa mda mfupi tangia awe mmiliki wa klabu hiyo.Chelsea imekuwa bigwa wa ligi kuu uingereza kwa takribani misimu mitano ,ligi ya mabigwa ulaya mara moja na ligi ndogo ya Ulaya (Europa) mara moja FA na kombe la ligi na ngao ya hisani kwa kifupi amna kombe ambalo hawajawai kuonja.
Kuna taarifa mbalimbali zinazoiandama klabu hii ya Stamford Bridge haswa muendano wake wa klabu hiyo.
Ilifika kipindi kocha wa sasa wa Chelsea akakiri haogopi kufutwa kazi na klabu hiyo.
Mutaliano huyo alipata kibarua hicho baada ya kumalizana na Italia katika euro michuano ya bara ulaya kwa nchi katika majira ya kiangazi ya 2016 msimu wake wa kwanza alitwaa taji la ligi kuu Uingereza huku akiongoza timu hiyo katika mechi 9 za ushindi bila kufugwa goli lolote na 13 bila ya kupoteza.
Anadai ya kuwa hashirikishwi kabisa katika masuala ya usajili , alianza kulalamika tangia mwisho wa msimu uliopita hapewi pesa na nguvu ya mawazo kwenye usajili.
Inakuwa ngumu kwake kuwapata wahitaji wake klabu hii ndo kocha wa kwanza analalamika hapewi ushirikiano kwa Mourhinho aliyeitumikia klabu hiyo katika nyakati mbili tofauti alikuwa na nguvu kubwa ya kunena linapokuja haswa suala la sokoni .
Haya yalisemwa na rafiki wa Antonio Conte wa karibu anaitwa Gianluca Viali.
Kuna taarifa zinasema ya kuwa hakuhusishwa kabisa katika uuzaji wa kiungo wa kati kwende Manchester united Mserbia Nemanja Matic anayefanya vyema huko Old Trafford.
Pengo lake halijazibika na Mfaransa Bakayoko mpaka siku za mwishoni walivyochukua uamuzi wa kumleta kiungo wa Leicester Drinkwater.
Na bado kuna upenyo Kante husumbuka haswa pale anapocheza na viungo wengine ambao hawana mbele wala nyuma
Haya kuondoka kwa mkurugenzi wa usajili Michael Emenelo Chelsea ambae alikuwa mtu muhimu sana na alikuwa nyuma ya mafanikio ya klabu hii,Pia kulitia shaka kuna ishu inaendelea nyuma ya pazia na baada ya mda akitimkia tena kule Monaco akipata ofisi hiyo hiyo huko Monaco .
Swali gumu je Michael aliondoka Chelsea kwa sababu gani mpaka naongea sasa amna mrithi rasmi isipokuwa mkurugenzi mkuu ameikaimu ofisi kwa muda na ndo anatoa sheria na kanuni mpya za usajili! kwa nini Michael aondoke ghafla?
Na klabu hii imetoa taarifa zikisema huenda mrithi akapatikana kabda ya msimu ujao kuanza.
Chelsea inakoelekea ni kwenda kuhangamia au kushuka kiuchumi na kimaendeleo ata dalili za kushuka kimaendeleo ya Soka zishaonekanana.
Msimu ujao wanatarajia kuupanua uwanja wa Stamford Bridge pia wakati huo huo wana mpango wa kumuondoa Kocha ambaye atatakiwa kulipwa pauni 9 milioni huku kukiwa na nyingine ya kumpa nafasi zaidi amalizie msimu ujao huko maana wanaona wenyewe ndo wana makosa kwani hawakumpa nafasi katika masoko ya ununuzi wa wachezaji. Hiyo ni sinema tu machoni mwetu.
Pia kuna wachezaji takribani tisa hatima yao inabidi ifanyiwe kazi katika majira ya kiangazi tukianza na mbeligiji Edern Hazard anatakiwa kuongezewa mkataba na mshaara tu mkubwa kwani mkataba wake upo tamaati 2020, Pedro ,Fabregas wanaoitaji mikataba mipya ikiwa bado msimu mmoja na Courtous anayeitaji kupewa mkataba wa maana, David Luiz naye kama wataitaji huduma yake mazungumzo yawe juu zaidi, Huku mbrazili William mkataba wake una misimu miwili tu unabidi ufikiriwe pia. Hao ndo wanabidi wapewe nafasi ya juu zaidi.
Huku wana itaji mshambuliaji wa kati atakayeweza kuziba pengo la Diego Costa .
Inaaminika Chelsea anaitaji kufanya mabadiliko makubwa zaidi ambayo yajawai tokea tengia mwaka 2003 na kuna itaji mipango na nafasi ya kocha katika soka wanaitaji kumsikiliza kocha kwani kocha ndo mwamuzi mkuu .
Nafasi za nne za juu msimu huu labda itokee tu kwa bahati mbaya lakini Chelsea anaitaji nguvu ya ziada ili kupata nafasi nne za juu.
maana gape lililoko ni alama 8 katika michezo 6 ni ngumu kwa kweli .
Kocha Antonio Conte ni bora lakini hana waitaji wake anaowataka pengine yuko nusu fainali FA kwa mara ya pili mfululizo ndani ya misimu miwili ni kitu bora kwa muitaliano huyu.
UCHAMBUZI na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni