Kocha wa Manchester city Pep Guardiola kafichua kuhusu kupewa ofa ya kuwasajili Henrikian Mkhtarian na Paul Pogba katika usajili wa dirisha dogo januari mwaka huu na wakala Mino Raiola.
Hayo yalitokana na wakala huyo kumkashifu kocha huyu wa klabu ya Manchester city kuwa "mbuzi na mbwa".
Wakati huo Guardiola akajibu mapigo kwa kusema ya nini kumkashifu na kumtukana wakati alimpa ofa za wachezaji hao januari mwaka huu.
Guardiola alisema "Naweza nikamjibu (Raiola) nashidwa kuelewa mimi ni mbaya kwa nini ,ni maoni yake kuhusu mimi ,nashidwa kuelewa".
Paul Pobga amekuwa gumzo klabuni Manchester united siku za karibuni anatarajia kusafiri na kikosi cha united kupambana katika mechi ya watani wa jadi wao Manchester city.
Hernkian Mkhtarian alitimkia klabuni Arsenal kwa usajili wa kubadilishana wachezaji ambapo Sanchez alitimkia united.
Taarifa hii imetoka kukiwa na presha ya pambano kati ya Manchester city na united ambapo city atatawazwa bigwa iwapo atapata ushindi kwa mara ya tatu ligi kuu uingereza na mara ya tano kiujumla katika historia ya nchi hiyo.
Habari na Prosper Bartholomew.
Simu :+255716243875.
barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni