Mshambuliaji wa Real Madrid na nahodha wa Ureno Christiano Ronaldo ameendelea kunyeshea nyavu katika ligi ya mabigwa Ulaya akiweka takwimu mbalimbali za soka katika maisha yake na soka la Ulaya.
Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michezo yote mtawalia kuanzia makundi mpaka robo fainali hatua ya kwanza ,ana magoli 14 katika michezo 9 aliyoitumikia bigwa huyu mara mbili mtawalia.
Ronaldo katika mashuti 10 aliyoyapiga yakimuekekea Buffon 9 yameingia golini na kuzaa matunda hiyo ni rekodi inayoshikiliwa na mshambuliaji huyo wa Ureno hasa ukilinganisha na golikipa wa aina hii ya dunia.
Sasa Ronaldo kafunga magoli 9 dhidi ya Juventus kuzifikia rekodi yake mwenyewe dhidi ya Bayern Munich na Lionel Messi dhidi ya Arsenal katika ligi ya klabu bigwa barani Ulaya.
Kiungo Isco Alaricon jana aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza duniani kutoa pasi 10 na kuendelea zikawa na 100 accuracy alitoa pasi 54 na aliushika mpira mara 68 akichezewa rafu 4 na ali drible mara 1 na akatoa pasi ya bao 1.
Ni kwa mara ya kwanza Juventus anapoteza mchezo mwaka 2018 baada ya kucheza michezo 16 bila ya kupoteza ikiwa alishinda 14 na kutoa sare 2.
Klabu ya Juventus imepoteza mchezo katika uwanja wa nyumbani katika ligi ya mabigwa baada ya kucheza michezo 32 bila ya kupoteza.
Kipigo cha 3-0 kinakuwa kipigo kikubwa kwa Juventus katika uwanja wa nyumbani tangia waamie hapo septemba mwaka 2011.
Takwimu na :Prosper Bartholomew.
simu :+25516243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni