RONALDO ATOA YA MOYONI KWA MASHABIKI WA JUVENTUS


Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester united na Sporting Lisbon anayeitumikia kwa mafanikio klabu ya Real Madrid amefunguka na kusema kuhusu goli lake lilozua kizaa zaa kikubwa katika ulimwengu wa soka kwani wengine wanasema ni goli bora la ligi ya mabigwa Ulaya la muda wote na kwa kweli kuna uwezekeo likawa hivyo.

Katika mahojiano na UEFA baada ya mchezo huo wa jana usiku alisema

"lilikuwa goli nzuri" ninachoweza sema lilikuwa la kusisimua"
Baada ya kufunga goli la Overhead kick kwa kutema yai.

"sikuwai fikiria ningefunga , tuachane nayo tuongelee kuhusu mchezo"

"Nafikiri mchezo ulikuwa mzuri na tumefanikiwa kufunga goli tatu dhidi ya Juventus,timu bora"

"Tulicheza vizuri na mimi nafuraha pia"

"Nilisaidia timu na kufunga goli mbili ulikuwa usiku mzuri"

Katika hali ambayo ijawai mtokea maishani mwake kwa kadiri nilivyomnukuu  amesema ya kuwa ajawai ona mashabiki wa timu pinzani wakimfanyia Juventus wakichomfanyia.

"Nataka kuwashukuru masahabiki wote wa Juventus,kwa kunifanyia kitu ambacho sijawai fanyika katika maisha yangu ya Soka"

Kuhusu Real Madrid kuwepo kwenye mbio za kushinda taji mara tatu mtawalia alisema

"Hili ni shindano letu" "Napenda sana kucheza huku"

"Ni matokeo mazuri,tunabidi kuwa makini katika marudiano"


Habari na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni