REAL MADRID YAACHA HASARA HUKO JUVENTUS

Kinachoongelewa katika mitandao ya kijamii ni kuhusu goli alilolifunga Christian Ronaldo dhidi ya Juventus usiku ambalo wanaliita Overhead kick katika ushindi wa 3-0 katika ligi kuu ya mabigwa Ulaya.

Mabigwa hao wa Italia walipata hasara katika soko la hisa kutokana na kipigo hicho cha juzi usiku kutoka kwa bigwa mtetezi Real Madrid.

Wamepoteza thamani ya asilimia 5 katika soko la hisa kutokana na kipigo hicho katika uwanja wao wa nyumbani.

Kuanzia saa saba kamili kwa mda wa Ulaya Juventus ilikuwa imepoteza hisa za asilimia 5.36 huku thamani ya hisa moja ikiwa 0.626 euro.

Na asubuhi ya saa tatu kamili mda huo huo wa Ulaya ya kati hisa zilishuka mpaka chini kabisa moja ikiwa inauzwa 0.615 euro.

Makala na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni