Kocha wa zamani wa klabu za Crystal Palace na Newcastle united ametimuliwa klabuni West Brownion Albinion baada ya kutokuwa na matokeo mazuri katika mechi za ligi kuu uingereza .
Alitua klabuni hapo Desemba mwaka jana na ameiweka klabu hiyo katika mazingira ya lazima kushuka daraja msimu huu wapo nafasi ya 20 wakiwa wamekusanya alama 20 katika michezo 32 msimu huu ikiwa imebaki michezo 6 tu kabda msimu huishe.
Katika hali hiyo amekuwa kocha wa kwanza kufukuzwa kazi siku ya jumatatu ya pasaka.
Atakayekalia kiti chake kwa mda ni kocha wa kikosi cha kwanza Darren Moore na atakuwa kocha wa hapo kwa mda .
Mada na : Prosper Bartholomew
simu: +255716243875.
barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni