Klabu ya Manchester united imewafurahisha mashabiki wake baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili na kurudisha yote na kuongeza moja zaidi katika ushindi wa 2 kwa 3 dhidi ya mahasimu wao Manchester city.
Paul Pogba alijikuta ndani ya neti katika uwiano wa sekunde 97 kabda Smaling kufanya ule msemo usemao goli la beki hudumu mkilichekea na ikatokea hivyo.
Manchester city alikuwa akishinda anatawazwa bigwa wa ligi kuu uingereza ukweli ni kuwa alijitakia kutokuwa bigwa katika siku kama ile ya watani wa jadi maana suala la soka alikuwa akilicheza ni sawa na kuchezea shilingi katika tundu la choo Sterling alifosishwa kucheza namba ya mshambuliaji wa kati wakati wote Jesus na Aquero wakipuumzisha misuli kwa ajili ya jumanne katika mechi ya marudiano ya mabigwa ulaya Sterling alikosa nafasi tatu za wazi za kufunga mabao huku Gundogan akifanya hivyo mara tatu licha ya kufunga bao safi aliyemzungusha Matic na kufunga.
Kwa nini Guardiola asingetoa sacrifice ya mmoja maana kazi ya Bernando Silva sikuiona uwanjani kabisa kuanzia dakika ya kwanza tukiachana na kukosa goli kwa mpira alioutelezea angempa nafasi mshambuliaji mmoja wa kati nafasi wangepata faida ya mabao mengi.
Suala la Guardiola kupoteza mchezo muhimu kama ule ambao umevunja rekodi yake na kuwa ameshafugwa nyumbani kwake katika ligi kuu uingereza kwa msimu huu ambao klabu ni hatari na kwa mara ya kwanza anaruhusu goli sita wavuni kwa takribani wiki moja tu. Ikiwemo nyumbani na ugenini .
Manchester united walivurugiwa plani na Guardiola kucheza kwa Herrera na Matic ilikuwa ina maana kazi ya Herrera ilikuwa kutibua mipango ya Bruyne na baada ya kuingia katika mchezo na kumkosa Bruyne Silva D. na Gundogan I. walikuwa wanapenya tu maana Herrera alicheza mpira mbovu kipindi cha kwanza ikiwemo kuruhusu mpira uchezwe kwenye zone ya united ambapo pogba alijiongeza na kurudi kama namba nane aliyekuwa mbele ilibaki lukaku na huku Sanchez na Lingard wakipotea maana namba kumi ilikuwa imekufa apo ujue Mourhino aliyekashifiwa na shabiki wa city kama empty mind na Guardiola Genius huyu Mou alihitaji dakika ata chache na kikosi kizima kupanga maelekezo na wajibu mpya maana mda mwingine Matic alicheza nane na sita huku Herrera ajui afanye nini uwanjani kengele ya kipindi cha kwanza ilivyoisha hapo ndo pakawa turning point ya Mourhino.
City angetumia nafasi alizozipata kipindi cha kwanza united alikuwa ameshaogelea namba maana timu ilikuwa inacheza ovyo ya united.
Baada ya kipindi cha pili Herrera akapewa kazi na maelekezo mapya na Pogba pia akarejea nafasi ya ushambuliaji ambapo nafasi zote zilimkuta alipostahili awepo amna ata goli la (bu bu) maana goli lilifugwa pale namba kumi anastahili kuwepo na kuwachanganya mabeki wanamkamara namba tisa wakati u kiungo mshambuliaji unaanjwa free .
Na ukiangalia goli la kwanza Herrera alicheza kama namba nane si mkata umeme akipochagwanywa na plani za Guardiola.
Mourhino akili yake alijua kwenye mpira ya kunyanyua City beki ilivyokuwa zembe kwa mipira hiyo cheki basi ya bao la kwanza la Pogba Delph ajui cha kufanya baada ya kunyanyuliwa huku goli la pili la pogba ikiwa Otamendi na Kompany walivyokuwa wanashangaa mpaka Pogba kujituma kwa kuruka kwa mbali kichwa cha kujituma .
Goli la Smaling la mpira uliokufa ulinyanyuliwa city beki hawakumaki mtu Guardiola anatumia soft ball sjui ya kutomaki washambuliji wakati wa mipira iliyokuwa Delph ajakamata mtu wakati wa faulo kwa nini Smaling asimtende mtu.kama anatoa maelekezo si kwa kutomakiwa kwa wachezaji vile iwe funzo City beki yake ijatulia ikawa tulii haswa huyu beki wa kushoto Delph.
Mourhino msimu ukiwa unaanza alikuwa anaomba timu yake iwai kufugwa alaf warudishe washinde lakini kimetokea tena kwenye mechi ya ajabu na haswa katika mechi ya watani wa jadi furaha kuanzia dakika ya 50 alipokuwa ameshapigwa 2-0.
Mourhino akikutangulia usitarajie kufika ndo alichofanya baada ya kupata goli la tatu alimfundisha soka Guardiola kuwa tunarizikaga na haya mambo McTominial aliweka njia ya kuongeza nguvu pale kati na pogba kurudi kama nane na City aliaibishwa machoni mwake ata akishinda taji atamsahau United na majogoo wa anfield.
Wafungaji wa Manchester city Vincent Kompony na Ikay Gundogan.
Wafungaji wa Manchester united
Paul Pogba mawili na Chriss Smalling.
Uchambuzi na Prosper Bartholomew
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni