KOCHA MSAIDIZI WA ANCELOTI AKIWA CHELSEA AFARIKI.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Ray  Wilkins amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Kiungo huyo aliecheza mechi 84 katika timu ya taifa ya Uingereza alianguka na kupelekwa hospitalini kusini mwa London.

Alikuwa akifanya kazi katika vyombo vya habari vya Skysport na Talk sport.

Amechezea timu 12 katika maisha yake ya soka huku akipata nafasi za ukocha usaidizi katika timu hizo.Na mojawapo ya timu hizo amekuwa kocha mwangalizi.

Aliitumikia miaka 6 klabu ya Chelsea kama mchezaji na amekuwa chini ya kocha Carlo Ancelotti kama kocha msaidizi klabuni Chelsea .

Carlo Ancelotti alishawai kumuita kama ana damu ya blue ndani yake wakati akiwa anafanya nae kazi.

Alishinda taji la FA mwaka 1998 na Manchester United na kombe la Scottish akiwa na Rangers.

Habari na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875
Baruapepe:barthaprosper@gmail.com

Maoni