GUARDIOLA NJE YA BARCELONA KALOGWA

Katika ligi ya mabigwa barani Ulaya Guardiola alichukua kombe lake la tatu na medali mwaka 2012 na Barcelona akaondoka Catalonia na kuenda kutafuta maisha pengine na kumeonekana kila dalili ya kumekataa huko kwingine katika ligi ya mabigwa Ulaya.

Baada ya kipigo cha kushitusha cha 3-0 kutoka kwa majogoo wa Anfield hamna ubishi kikosi cha Guardiola kinaitaji kufanya kazi ya ziada katika marudiano ya mchezo wa raundi ya pili.
Ijulikane ya kuwa moja ya sababu ya kuletwa Guardiola kwa wananchi ni kutafuta kombe la ligi ya mabigwa Ulaya.

2013-14. Alitua Ujerumani Bayern Munich kuchukua mikopa ya Jupp Heyckens aliyestaafu licha ya kurejea tena katika kiti hicho kuanzia mwezi wa 10,2017. Munich walikuwa mabigwa watetezi wa kombe hilo kilichomsibu ni historia kwake kwani Mhispaniola huyu alipigwa agregate ya 0-5 na mpinzani wake wa Hispania Real Madrid ikiwa ni nyumbani kwake hiyo ilikuwa hatua ya nusu fainali .
Philiph Lahm alinukuliwa akisema "Guardiola alituita sita yetu na kutuuliza tulitaka tuchezaje".

2014-15: Hapa alishidwa kukwepa timu yake ya zamani na pedwa alitamani kuonesha kuwa yeye hujua na alitaka kuwacharaza mpaka timu yake hiyo kilichogeuka ni kilio cha kusaga meno ilikuwa katika hatua ya nusu fainali alipomenyana na Barcelona ni aggregate ya kufugwa 3-5 hapo alijitahidi vya kutosha kupata magoli matatu lakini alishidwa kuzuia matano tena.
"Tulianza vizuri , vipaji vyao vikafanya mabadiliko " Baada ya Bavaria kupigana na kushinda 3-2 katika mechi ya marudiano Alianz Arena licha ya kupoteza 3-0 comp nou.

2015-16:Alitupwa nje kwa aggregate ya bao 2-2 moja likifugwa na Saul Niguez dimbani Vincento Golderon katika ushindi wa bao 1-0 wa Atletico Madrid.
Na Bayern alishinda nyumbani bao 2-1 na goli la Graizeman lilihakikisha huyu mhispaniola aonji fainali ya ligi ya mabigwa Ulaya na Bayern.
Wote walimfanyia vituko akiwa na Bavarian walikuwa Wahispaniola tena katika nusu fainali.
Waongeji hatukosi maneno yaliyomtoka yalikuwa "Mda wangu klabuni hapa utajadiliwa kutokana na kutofika fainali"
"Ningeumizwa kama hatukucheza vizuri ,lakini tulifanya " maana alijua ulikuwa mwisho wake jijini Munich.

Lipicha la Bayern la misimu mitatu likaishia hapo.

2016-17: Alitua klabuni Manchester city akiwa ametoka kuchoshwa na Bayern kazi ya kwanza nikuipeleka Manchester city angalau fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake mtangulizi wake alisaidia ifike nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu licha ya kutolewa kwa bao moja kwa bila na Real Madrid.
Katika hatua za awali tu na Monaco ya Ufaransa ilimsumbua kichwa walitoa suluhu ya 6-6 na alitupwa nje kwa magoli ya ugenini ,hii ilimfanya kuendeleza rekodi mbaya akiwa nje ya klabu ya Barcelona .
Meneno ya kuwapinga wakosoaji wake yalikuwa "Tunajifunza kupitia makosa ,Kikosi hiki hakina experience kwenye michuano hii" akiwa ametumia pauni 213milioni kwa mara ya kwanza tu alipotua hapo huku Monaco wakicheza na vipaji vidogo kina Mpape,Bakayoko,Fabinho.
"Tutakuwa wazuri licha ya haya mashindano kuwa magumu"

Makala na Prosper Bartholomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni