FERNANDO TORRES NA ATLETICO MADRID MAPACHA AMBAO WAJAONJA TUNDA PAMOJA

Baada ya siku 6,161 baada ya Fernando Torres kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya leganes 2001 amethibitisha ataondoka tena mwisho wa msimu huu.

Baada ya misimu 11 klabuni hapo hana budi kuondoka ametoa kila msaada hasa akicheza ligi daraja la kwanza ,ligi kuu ,mabigwa ulaya ,Europa ,na kombe la mfalme.

Katika miaka hiyo yote mhispaniola huyu amecheza michezo 393 akishinda 186 akitoa suluhu 101 na kushuhudia vipigo 106. akianza michezo 299.

Katika michezo hiyo amejikuta wavuni mara 126. ikijumuisha mchezo dhidi ya Moscow Europa ligi mda si mrefu.

Amekutana na timu 66 na amezifunga 40 ya timu hizo na amekuwa muuaji wa Barcelona baada ya kuwa anaongoza timu hizo kwa kuifunga akiwa amefunga 10 dhidi ya 21 alizocheza nazo.

Amekutana na sura 134 mpya katika vyumba vya kubadilisha nguo huku akikutana na Gabi katika vyumba hivyo mara 174.

Amekuwa chini ya makocha takribani wanane wakiwamo Diego Simeone , Luis Aragones , Gregorio Monzano , Javier Aguirre , Bianchi , na Pepe Maurcia.

Kwa sasa kuna michezo 11 imesalia kwa Atletico Madrid huku akionekana ana uwezo wa kufikisha michezo 400 katika klabu hiyo na goli 100 za laliga ambapo kwa sasa ana goli 99.

Itakuwa bora kama watashinda nako taji la Europa kwani anasuburia kushinda taji lake la kwanza na klabu aliyoitolea kila kitu tangu alipokuwa mdogo.

Takwimu na Prosper Barthalomew.
Simu:+255716243875.
Barua pepe:barthaprosper@gmail.com.

Maoni