CHELSEA KUMPOTEZA WINGA MWINGINE TENA ,SASA NI MBRAZIL

Winga Mbrazili Robert Kennedy Nunes (22) anayeitumikia kwa mkopo klabu ya Newcastle united amekuwa gumzo barani Ulaya kwa kila klabu kumtaka.

Tengia atue klabuni Newcastle amekuwa na madhara makubwa ukilinganisha amechangia magoli mawili na kuzaa mawili katika mechi nane alizoichezea Newcastle kuanzia januari huku wakiamini watampata jumla katika majira ya kiangazi.

Chelsea imekuwa ikimtumia mara chache ukilinganisha na kiwango alicho nacho huku akisugua benchi kwa Marcos Alonso pia anaweza tumika kama mshambuliaji wa kati kiungo mshambuliaji na beki kwani Chelsea ilishawai mtumia kama namba tatu beki ya kushoto pale Jose Mourhinho alivyokuwa kocha wa blues mda mwingine winga na kiungo nafasi hizo alizitumikia msimu wa 2015-16 pale wachezaji wa blues walikuwa wachovu na chini ya kiwango.

Klabu za Bayern Munich na PSG wameuliza klabu ya Chelsea kama kuna maendeleo ya kumuachia katika majira ya kiangazi huku amna ofa iliyoko mezani tayari.

Arjen Robben na Frank Ribery mikataba yao inaisha msimu huu na wanatafuta watakaowarithi kwa muda mrefu kama walivyoitumikia klabu hiyo.

Klabu ya Chelsea ilimnasa kwao Brazil 2015 klabuni Fluminense na ameitumikia Chelsea katika michezo 15 ukijumlisha na ligi ya mabigwa Ulaya 2016 dhidi ya PSG alitokewa kwa mkopo mwanzoni mwa 2016 klabuni Watford alikocheza mchezo mmoja tu na alitokea benchi Chelsea ilimuita nyumbani na msimu huu ilimtumia katika michezo ya kombe la ligi na FA kabda hawajamtoa kwa mkopo januari hii huko Newcastle.

Habari na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875.
barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni