ANDE HERRERA SI MAKUSUDI

Kiungo mkata umeme ameamka na kujitetea kwa kitendo kinachoongelewa katika mitandao ya kijamii kuwa aliikanyaga nyaga na kuidharau nembo ya klabu ya Manchester city iliyoko mlangoni pa kutokea na kuingia uwanjani.

Baada ya timu yake kupigania na kufanya mapinduzi kutoka nyuma ya 2-0 mpaka kushinda 3-2 katika watani wa jadi wa Manchester.

FA shirikisho la kandanda Uingereza likithibitisha halitamshughulikia kwa kitendo hicho.

"Daima nitaipigania nembo ya klabu yangu na pia nitaheshimu nembo nyingine za klabu hizo" Alisema hayo katika mtandao wake wa kijamii wa instagram pia msemaji wa klabu ya united hakikata kusema kuwa ilikuwa plani ya mchezaji baada ya kitendo.

Habari na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875.
Barua pepe:barthaprosper@gmail.com.

Maoni