MFUMO WA MAAMUZI YA VIDEO (VAR) KATIKA SOKA UNAVYOFANYA KAZI :

Wapinzani wa mfumo huu wa msaada wa Video kwa muamuzi (VAR) wanasema mfumo unachelewesha mchezo lakini ukweli mfumo unatumika pale mchezo unaposimama na unatumika sana katika vipengele vinne muhimu katika soka haswa vipengele hivyo vikiwa utata katika goli,penati,Kadi nyekundu ya moja kwa moja na utata ulionekana.
Pale ambapo maamuzi yamefanywa na mfumo huu muamuzi anachora kiboxi kwa mashabiki kinachoashiria TV kuonesha maamuzi yamefanywa na VAR. Ijulikane kuwa muamuzi mwenyewe au VAR huenda ndo wameomba tukio lifanyiwe uchambuzi zaidi au kurudiwa.
Mashabiki walioko uwanjani hawataonesha marudio ya matukio lakini waangalia nyumbani wataoneshwa kama refa anavyoona kwenye marudio  ili kupata kitu kinachoendelea wasiwe nyuma na mfumo huu.
Mfano mchezaji amefunga goli la kuotea na refa ameona kama goli VAR itamjulisha kuna kosa limetokea kwamba mchezaji ameotea muamuzi atachora kifaa kama TV na kubadilisha lile wazo la kwanza na kuweka wazo nyingine,hii ni njia mojawapo ya uamuzi .
Nyingine ikitokea utata VAR watamshauri kwenda kuangalia kitu kinachoitwa "on- field review " kwa kimombo hapo sasa muamuzi atasogelea miguu yake pembeni mwa uwanja na kuanza kuangalia monita ambayo ina video ya utata kabda ya kutoa maamuzi.
Makala na Prosper Bartholomew.
simu :/+255716243875.
barua pepe : barthaprosper@gmail.com.

Maoni