DAVID SILVA AELEZA MATATIZO YANAYOMSIBU

Kiungo mchezeshaji wa Manchester city David Silva aliyekuwepo nje ya uwanja kwa muda katika kikosi cha Manchester city amefunguka na kutoa sababu maalumu ya kuwa nje ya kikosi hicho ni kutokana na matatizo ya kifamilia.
Mhispaniola huyo alipewa ruhusa maalumu hasa muda wa krismasi kwenda katika nchi ya nyumbani Hispania kukaa na familia yake na mtoto wake Mateo ambaye hakuzaliwa vizuri. na mkewe Jessica Suarez.
Baada ya kurejea katika kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola kilichoshinda mabao matata kwa moja jumatano jioni dhidi ya Watford   baada ya kupata suluhu dhidi ya Crystal Palace.
Na anatarajiwa kurejea nchini Hispania tena siku za karibuni.
Silva alisema "Nataka kushukuru kwa upendo wenu na ujumbe mzuri niliopokea kwa wiki kadhaa , shukrani za upendeleo kwa wachezaji wenzangu na kocha wangu na wote "
"Pia nataka kuwajulisha kwa mtoto wangu Mateo aliyezaliwa na shida anapigania  siku hadi siku pamoja na msaada wa bodi ya madaktari"
makala na Prosper Bartholomew
simu :/+255716243875.
barua pepe (EMAIL): barthaprosper@gmail.com

Maoni