JOSE MOURINHO AFUNGUKA KUHUSU HATIMA YAKE KLABUNI MANCHESTER UNITED

Kocha José Mourinho amepuuzia uvumi unaomlenga kuwa ataondoka klabuni Manchester united mwisho wa msimu huu katika kipindi cha  majira ya joto .

Kocha huyu wa old Trafford amebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika kandarasi aliyosaini mnamo majira ya kiangazi 2016.
Tayari ashaanza kuangalia uwezekano wa kupewa kandarasi ya muda mrefu kwa klabu hiyo iliyoko kaskazini magharibi mwa Uingereza Jijini Manchester.

"Lengo langu ni kubaki , na kufanya kazi na kupeleka klabu pale ilipokuwa na nataka kubaki , sioni sababu ya kutobaki "

Mreno huyu yupo katika hatua za mwanzoni za kuongeza mkataba na makamu mkurugenzi Ed  Woodward na ana amini kuwa ataendelea kubaki katika kandarasi yake ya sasa.

"Ndio,nitaona mwenyewe , narudia ni swali la klabu , bodi , na wamiliki na bwana Woodward , wote wanataka na wanafurahi na mafanikio niliyoyafanyia klabu hii "

Katika kipindi cha msimu mmoja na klabu hii ametwaa taji la europa ligi na kombe la Carabao msimu uliopita pamoja na ngao ya jamii katika msimu wake wa kwanza , katika msimu huu anashika nafasi ya pili katika ligi kuu uingereza pamoja na yuko katika raundi ya 16 bora ya ligi ya mabigwa ulaya pamoja licha ya kutolewa nje ya kombe la Carabao.

Kocha huyu anahusishwa kutokuwa na furaha na klabu hii katika suala la usajili alilolilamikia katika wiki za karibuni,anaishi katika hoteli badala ya kununua jumba la kuishi kama kweli atabaki Manchester united lakini katika mkutano wa leo kuelekea mchezo wa kombe la FA amesema jukumu lake ni kufanya kazi si kulinganisha na stori potofu 

Klabu ya Manchester united inatarajia kuanza kampeni yao nyingine katika kombe la FA kesho ijumaa dhidi ya Derby kukiwa na matumaini baada ya kurejea kwa Romelu lukaku na Mouroine Fellaini wote kutoka majeraha na Romero anatarajia kutoa msaada golini kwa David De gea .

Makala na Prosper Barthalomew .
simu :/ +255716243875.
barua pepe : barthaprosper@gmail.com

Maoni