Kocha wa Barcelona Ernesto Valvede ambaye kwa sasa timu yake inaongoza ligi nchini Hispania kwa tofauti ya alama nane ikiwa ijafugwa bado michuano yote inayoshiriki msimu huu.
Ikiwa Neymar aliondoka Barcelona ikiwa inaingalia Real Madrid iliyotwaa Laliga pamoja na ligi ya mabigwa ulaya na kupigwa mara mbili katika supercup ya Espanol ilikuwa mda mgumu sana kwa klabu kama klabu na mashabiki.
"Kuondoka kwa Neymar kulikuwa kubaya sana kwa klabu na muenendo wake"
"Hatuwezi kukataa hilo " Valvede akiwa anaieleza tovuti ya Barcelona katika mahojiano.
Baada ya Barcelona kuondoka kwa staa wake walifanya usajili wa kumleta kinda wa Ufaransa Ousmane Dembele ambaye alipata majeraa tu katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuanza dhidi ya Getafe ambapo anatarajiwa kurudi na kucheza mchezo wowote kuanzia sasa hivi bado ajafunga goli lolote katika klabu hiyo.
"Tunajua Messi anaweza cheza nafasi yoyote lazima tumpange pale
atakapofanya mashambulizi yetu "
"Tunabidi kuangalia nafasi ambazo Messi na Suarez wanazicheza "
Licha ya vichwa vya habari kuhusu Countinho zikielekea kuhusu uhamisho wake kutua klabuni hapo lakini Kocha Valvede amesema kurejea kwa Dembele ni muhimu kwa Barcelona.
"Kuwa mchezaji wa Barcelona unabidi uwe na sifa mbalimbali "
"Dembele anabidi kuzoea , jeraha lake ni kubwa sana , likikuwa kubwa"
"Ni mdogo na amejaliwa kipaji, lazima kutakuwa na mtazamo mkubwa sana kwake baada ya usajili mkubwa"
Makala na Prosper Bartholomew.
Simu :/ +255716243875
barua pepe :( EMAIL) : barthaprosper@gmail.com
Maoni