Klabu ya Liverpool ilifanikiwa kuinasa rasmi saini ya beki wa kati Virgil Van Djick kutoka kwa klabu ya Southampton kwa dau la pauni 75 milioni sawa na bei ya kununulia washambuliaji hatari wa kati kama Romelu Lukaku na Alvaro Morata .
Wakiweka rekodi ya dunia ya beki ghali zaidi Ulimwenguni kununuliwa wakipiku rekodi ya John Stone wa Manchester city na Bonnuc wa Ac Milan.
Liverpool imekuwa ikipata matatizo mengi katika ulinzi wakiwa wanarudushiwa magoli katika michezo mbalimbali mfano mechi dhidi ya Sevilla uwanjani Sanchez walipokuwa wakiongoza mabao 3 na kurudishiwa yote katika mchezo wa ligi ya mabigwa ulaya ,na dhidi ya Arsenal walipofugwa magoli matatu kwa sekunde 388 juzi ijumaa.
Katika miaka minne ya Karibuni Liverpool wamekuwa wakivua wachezaji mbalimbali kutoka kwa Sauthamptom ikiwemo beki wa kati Dajen Lovren aliyenunuliwa kwa pauni 25 milioni pamoja na beki wa pembeni Nathaniel Clyne , Rickert Lambert aliyefunga magoli 4-3 tu klabuni hapo kabda ya kutimukia West brom , Sadio Mane .
Dajen Lovren amekuwa akionekana butu sasa huenda akaungana na Virgil van Djick au apoteze namba kwa beki huyu .
Kuchelewa kwa kufikishwa jina katika bodi ya Ligi kuu uingereza atacheza dhidi ya Burnley badala yake atacheza kwenye kombe la FA katika mchezo wa Merseyside derby dimbani Anfield.
Lakini kumekuwa na minongono ikisema Liverpool wametumia hela ghali sana kwa beki si wa fesha hiyo Ila kwa maoni yangu naona kama Liverpool asingetoa hii hela basi VVG angetimukia klabuni Manchester city ambapo mambo yangeanza kabisa kukata ladha .
Sasa klabu ya Liverpool inabidi imalizie kumleta Naby keita pamoja na beki mmoja wa kati na golikipa ili kuacha usindikizaji katika ligi kuu uingereza kuanzia mfumo mpya wa ligi kuu uingereza 1992 wajawai shinda taji la ligi kuu.
Nafikiri tatizo kubwa la Liverpool ni golini wamalize kumpata golikipa bora na kiungo mmoja wa kati na kuhakikisha wanasolve matatizo ya majeruhi kama kwa Henderson na wengineo maana kwa mbele ni moto si kawaida maana wakiobakia ni sehemu hizo maana Chermberlain ameshakuwa bora na Wjildnam naye yuko bora na Henderson wamalizie. matatizo manne yakiwemo majeruhi,kiungo mkabaji ,beki mmoja wa kati pamoja na golikipa .
makala na Prosper Bartholomew.
simu:/+255716243875
barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni