Kiungo mshabuliaji wa pembeni Kingsley Coman ameongeza mkataba klabuni Bayern Munich utakaomuweka hapo mpaka mnamo 2023 ,amekuwa chaguo bora kwa kocha aliyerithi kibarua cha Carlo Ancelloti Jupp Heynckes
Katika wakati huo huo mshambuliaji aliyekuwa anasumbuliwa na tetesi za kuhama klabuni TSG 1899 HOFFENHEIM kwenda Bayern Munich Sandro Wagner amerudi klabuni Bayern na kurambulishwa rasmi huenda akawa chaguo la pili mbele ya mpoland Lewandoski , Msimu uliopita alihakikisha anawapeleka kikosi cha Hoffenheim ligi ya mabigwa ulaya kazi iliyofanikiwa .
Katika mchezo wake wa kwanza wa kitaifa wa makundi ya kufuzu kombe la dunia akiwa na ujerumani alipachika mabao matatu yanayosemeka kama hat-rick .Amekabidhiwa jezi namba 2.
Licha ya kuwa bora ya kushinda mechi 16 mfululizo katika ligi kuu uingereza Kocha wa Manchester city Pep Guardiola anataka usajili wa Januari umlete beki wa kati ambaye hajatulia kabisa katika klabu ya Southampton Virgil van Djick ambaye ata hatumiki mara nyingi msimu huu kutokana na kutokuwa na uhakika wa kusalia klabuni hapo .
Pia Pep anahitaji kwa hali na Mali huduma ya mshambuliaji wake wa zamani klabuni wakiwa Barcelona Alexis Sanchez ambaye alikuwa akiyamaniwa sana katika majira ya kiangazi kocha Pep anataka kuweka ushindani mkubwa zaidi .
makala na prosper Bartholomew
simu:/+255716243875.
barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni