UCHAMBUZI:WILLIAM ALIVYOWASAFISHA CHELSEA , KOCHA WA BURNLEY KAWAPA NDOTO SAFI MASHABIKI,KOCHA DORTMUND KASAFISHA NYOTA.
BURNLEY 1-0 STOKE CITY:
Goli lilofugwa na Ashley Barnes dakika ya 89 ndo limewapa ushindi vijana wa Turf Moon na sasa hii timu imeweza pata alama 31 katika michezo 17 iliyocheza msimu huu chini ya kocha wao Sean Dyche na wametulia nafasi ya nne kabda ya michezo ya kesho
kocha wa stoke city Mark Hughes amesema Burnley hawakustaiki ushindi kwani timu yake ilichokicheza ushindi ulikuwa mkononi mwa klabu hii potters
Klabu hii ya Burnley huenda ikawa sumbufu kwa vilabu vikogwe na tayari ishaanza kazi kwani ilimkunguta kibano Chelsea na kupata suluhu dhidi ya Liverpool sasa inashika nafasi ya nne nyuma kwa alama nne namba tatu Chelsea
klabu ya Burnley imepanda nafasi kubwa sana katika ligi kuu tangu 1975
HUDDERSFIELD 1-3 CHELSEA
William ameweka rekodi yake ya kuchangia magoli yote matatu kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ligi kuu uingereza bao moja na pasi za mabao mawili .
kocha Antonio Conte ametumia mfumo wa 3-4-3 huku mbele Hazard Pedro na William wakisimama kama washambuliaji ameachana na mfumo alioutumia katika kipigo cha bao moj kutoka kwa West ham united baada ya kukos huduma ya majeruhi Alvaro Morata
William Borges amefanya dribbling 4 akapiga grosi 4 akatoa key passes 3 na kutoa assiti 2 na bao 1.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte anasema kitu ambacho hajakifurahia ni kufugwa goli dakika ya mwishoni wakati alihitaji clean sheet.
MAINZ 0 - 2 DORTMUND
Dortmund baada ya kumpa kibarua kocha wa zamani wa Koln Peter Soger baada ya kukaa na timu kwa siku kadhaa ameweza rudisha matumaini kwa mashabiki tena.
kwa kipindi cha kwanza Mainz walikuwa na mashuti 6 wakati hawa Dortmund walikuwa na mashuti 5.
Tatizo kwa upande wa Dortmund kwa siku za karibuni ni ulinzi usivyo imara unakatika Jana Mainz ilibidi ashinde Ila kipindi cha pili Dortmund alibadili mchezo na matokeo yakapatikana kwa kocha mpya huyu wa Dortmund
Kagawa bado bora kwani alicheza dakika 90 akishambulia akitia hofu katika lango la adui na katika midfield ya upinzani na alipachika bao la pili na kumpa ushindi Peter Soger katika mchezo wake wa kwanza Dahood aliingia kuubadili mchezo huku Abubeyang akiwa wa presha kwani goli la Kagawa alilijenga yeye
C.PALACE 2 - 1 WATFORD
Mchezo huu ulikuwa na raha yake Watford kaongoza zaidi ya dakika 85 kabda vijana wanaoenda kwa jina la Eagle wajapindua matokeo hayo.
Sasa wametoka katika mstari mwekundu kabda ya michezo ya leo kwa mara ya kwanza Kocha Hodgson anaona mambo yababadilika zaidi na kuanza kuwa mazuri Watford alipiga mashuti 2 on target Crystal palace akilenga goli mara nne
Goli la Bakary Sako lilikuwa la kusawazisha baada ya straika huyu kutokea benchi na goli la ushindi ambalo si rahisi kusahaulika kwa mashabiki hawa wa selhust park la James McArthur
makala na prosper Bartholomew
simu +255716243875
barua pepe:barthaprosper@gmail.com
Maoni