UCHAMBUZI:MWENENDO WA CHELSEA UTAFAKARIWE , REAL MADRID YA 4-4-2 ILIVYOMKUNGUTA MTU BUCHANI

WEST HAM vc CHELSEA- Klabu ya West ham baada ya kupata mateso mengi kwenye ligi kuu uingereza sasa wamepata ushindi wa kwanza chini ya Kocha David Moyes,
David Moyes ameongoza West ham katika michezo 5 ameshinda mmoja na kupata suluhu moja na amepoteza mechi tatu . West ham amekuwa akilinda sana ,na Chelsea kwa nafasi alizozipata kupitia kwa Morata na kuzikoza zimewaponza West ham alikanza kila sehemu baada ya kupata  bao dakika ya 6 kupitia kwa Autonovic alyebaki mbele alikuwa Antonio alyekuwa akiwasumbua mabeki kwa kipindi cha kwanza amegusa Mara 19 katika nusu ya uwanja wa ulinzi Chelsea katika mashambulizi kupitia mashambulizi ya Counter attack pamoja na goli west ham alipata attempt 4 kwa 9 katika kipindi cha kwanza .

Chelsea walifanya kila kilichowezekana kusaka ushindi au kusawazisha Ila walishidwa kupata chochote sasa kocha Conte ana kazi ya kukiongezea makali kikosi hicho  Alvaro Morata alipata nafasi nyingi za kupata bao Ila alishidwa akuwa na umakini mkubwa alikuwa awekezi akili nyingi uwanjani alikuwa achezi na timu anapata mpira anataka kuwa kama player maker anaishia kuweka mpira hatua moja mbili unachukuliwa mabeki kina Reid ,Cresswell ,walimuweza Kina Obgonna walimtuliza akitaka kudrive mpira ananyagwanywa alishidwa kucheza na timu yake badala yake alicheza mwenyewe William Moses na Pedro walishidwa cha kufanya mbele ya watu 8 mpaka 9 golini West ham walijirekebisha kutoka kwa makosa waliyoyafanya jumapili

Goli la West ham lilikuwa la kizembe Chelsea alikuwa na watu 8 wamevaa jezi nyeupe walishidwa kuzuia shambulio lile ambao hawakuwepo kwenye lile tukio ni Hazard Morata walimchekea Autonovic walishidwa kumzuia one two ya Autonovic ilizaa tunda lililokamilisha matokea Muastralia huyu alimpa kitu David Moyes 

Sasa Chelsea katika michezo 16 ya ligi kuu uingereza kapoteza minne sasa swali la kujiuliza kuna timu ya ubigwa inapata matokeo hayo kwrnye mechi zake 16 za kwanza cha kufanya tuelekeze macho kwa Manchester watani wa jadi alaf tutaongelea stori za ubigwa ubigwa kwa Chelsea nafikiri umepungua asilimia bigwa huyu mtetezi anabidi afikirie sana kukosekana kwa Drinkwater Bakayoko ameshidwa kuziba pengo la Matic bado Chelsea anazidi kuona uwanja unapwaya  sasa kutoka 3-4-3 mpaka 3-5-2 ili kujaza viungo nao wanashidwa

Nadhani ni mda mwafaka wa kuanza kufanya usajili wa maana kwa Chelsea kujaribu kuongeza makali Hazard ilifika mahali akarudi nyuma kutafuta mipira kutafuta sehemu walipofungua Bakayoko na Fabregas wakikuja kucheza nafasi moja kipindi cha kwanza kweli kutafakiri ni kitu cha muhimu kwa Chelsea kuna mda nyuma walibaki wawili wote wakapanda Christeanens na Cahill walibaki Azphiliqueta akaongezeka kushambulia amna kilichotokea tatizo la chelsea kwanza Morata kama nilivyomweleza Leo .

REAL MADRID vc SEVILLE : Uwanjani Santiargo Bernabeu hapakuwa salama hasa dakika 45 za kwanza ambapo mchezo ulikamilika

Kocha Zidane alikuwa akikosa huduma ya Verane ,Carvajal na Ramos hakuwa na namna alifanya uamuzi wa kutumia mfumo wa 4-4-2 Ronaldo na Benzema kama mastraika katikati akiwapa nafasi Vazquez ,Kroos Modric,Asensio huku nyuma akiwapa nafasi ya ulinzi Hamiri Carvelo,Nacho na Marcelo lakini kikosi hiki kilicheza mpira wa nguvu kupitia mashambulizi ya haraka goli la kwanza likipatwa dakika ya 3 Nacho Fernandez

Sevilla walipatwa na presha ya mchezo na iliwaendesha kipindi cha kwanza walisukuma mpira bahati walizikosa na kukubali kichapo, wakipofunguka Madrid alichukua mipira haraka na kumuwai na kumaliza . Ndio ugenini si wazuri sana kwani michezo 28 sevilla amecheza nyumbani hajafugwa akiwa Sanchez alishidwa kuutuliza mpira dakika za kwanza .Walikuwa hawajiadhari kama ni malalamiko beki wa kushoto aliumiza sana timu magoli yote yamepita uchochoro huo isipokuwa goli mbili . kwa nini wauweze mpira kipindi cha pili cha kwanza waushidwe  Jesus Navas Nolito Benaga na washambuliaji wao wengi wameshidwa Fanya lolote mbele ya timu kama vile ambayo mabeki hawakuwa watu wakubwa.

Marcos Ansensio anazidi kujiamini na kiwango kinazidi ongezeka , Amejenga magoli mazuri pamoja na nafasi nzuri kipindi cha kwanza goli la Ronaldo amemtengenezea vyema ni mchezaji mdogo wa kiwango kikubwa ana mda wa kuafuta makuu zaidi anaongeza kiwango kila anapopewa nafasi ana tia hamasa.Lucas Vazquez anaitaji kurudisha kiwango chake kuonesha tofauti kuongeza presha kwa mpinzani kama alivyo Ansensio kujaribu kuwapa nafasi ya kushinda wenzake si kutafuta mwenyewe kwanza

Kama mchezaji bora wa mchezo ni Ronaldo magoli mawili na amesaidia kwenye move za magoli mengine ni mchezaji bora wa dunia sasa miaka 32 bado anasumbua uwanjani . 

Madrid si wa kuchezea kwenye mashambulizi ya haraka amemua Seville 5-0  Archuf Hamiki ana miaka 19 na goli la kwanza katika jezi ya Los Blancos  .Toni Kroos kwa goli alilolifunga ni vizuri kwa kiungo Madrid ana mtu wa kusumbua barani ulaya pasi matengenezo ni nini amekosa Kroos ametafuta nafasi safi na kupata goli .

Makala na prosper Bartholomew
Barua pepe:barthaprosper@gmail.com
simu :+255716243875

Maoni