UCHAMBUZI : SOUTHCOAST DERBY ILIVYOKUWA NA UHONDO ,SIRI HII HAPA KWA NINI MAN CITY ANASHINDA DAKIKA 10 ZA MWISHONI
Katika ligi kuu pedwa ulimwenguni ligi kuu uingereza(EPL) kulikuwa na michezo miwili ili kukamilisha wiki ya 15
AFC BOURNEMOUTH VC SOUTHAMPTON:
Mechi ya kwanza ilihusisha Derby ya Southcoast ya uingereza na ni mechi mojawapo ya derby inayokuwa na raha na mwamsho mkubwa
Bournemouth kati ya Sauthamptom mchezo uliopigwa uwanjani Vitality Eddie Howe kocha wa Bournemouth alkuwa ana mkaribisha kocha ambaye ndo mchezo wake wa kwanza wa watani wa jadi iyo Pellegrino.Mchezo ulitoka suluhu ya bao 1 kwa 1 Franser alianza kufunga wa kwanza na kusawazishwa kwa goli na Austin
Mchezo ulikuwa mzuri kwani timu zote zikichezeana kwa awamu amna alyemzidi mwenzake.
kocha Eddie Howe ikiwa huu ni mwaka wa 9 klabuni hapo kama kocha na ni kocha mwenye umri mdogo katika ligi kuu uingereza na aliwapandisha daraja tengia apande daraja amekuwa ni kocha aliyekuwa akisumbua vigogo tengia kwani timu yake ilimfunga Chelsea Stamford bridge ikiwa imepanda daraja kiasi kilichotia hofu kwa kutimuliwa Mourhinho ilikuwa December 2016 1-0 goli lilifugwa na Murray kipindi cha pili , msimu uliopita alimtoa jasho jembamba mourhino alivyomkazia na kutoa nae suluhu ya bao 1-1 pale old Trafford licha ya Bournemouth kucheza pungufu kipindi cha pili.pia msimu uliopita Arsenal ilimbidi atoke nyuma kwa magoli matatu sifuri na kusawazisha tena Bournemouth walikuwa na kadi nyekundu , pia uwezi kusahau kipigo cha kutoka nyuma alichokipata Liverpool alipokuwa anaongoza 3-1 na kurudishiwa na kupigwa 4-3pale vitality. Hizi ni moja kati ya mafanikio a kocha huyu alyeitumikia klabu hii kama mchezaji piya msimu huu walianza vibaya Bournemouth wamekuwa wakiimprove siku na kila siku
katika mchezo wa Leo Defoe ambaye ana hatrick mbili dhidi ya Southampton alianzishwa kucheza mfumo wa washambuliaji wawili 4-4-2 wapinzani wageni walitumia mfumo wa 4-2-3-1 huku Redmond lemina wakiwa nje , Charries walikuwa wanakatika sana katikati licha ya kuwa na viungo wanne Romeu na Steve Davis waliwashinda wakiwa na possession Saints walikuwa wandurahisha huku Bertrand akiwa bora kwenye mashabulizi Tadic hakuwa katika kiwango bora ambacho kingeamsha hisia za watu ajawa yule kiumbe ambaye tumemzoea word powse alicheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni hupedwa kuitwa wing a alishidwa kuvuma mpaka kocha alivyomuingiza Redmond alyetoa pasi ya bao.
Column Wilson na Jordan Ibe wameingizwa dakika za mwishoni willson alifunga hatrick kwa Huddessfield akiwa ametoka majeraha Ila Bournemouth walishambulia sana Ila Forster na Begovic walifanya bora katika kuokoa timu zao, lemina mchezaji ghali zaidi kununuliwa katika historia ya klabu hiyo ajaonesha makali licha ya kuingia kipindi cha piki nafikiri anabidi aongeze bidii Mgabon huyo.
klabu hizi zimecheza Soka nafikiri matokeo yaliitajika kwenye mchezo yalibidi yawe vile.
MAN CITY VC WEST HAM :katika mchezo huu Manchester city alipata ushindi wa bao 2 kwa 1 west ham walikuwa wa kwanza kuandikisha bao kupitia kwa beki Ogbonnna na Otamendi kusawazisha kabda ya David silva kuwapa ushindi ikiwa dakika 10 za mwishoni za mchezo.
kocha David Moyes inaonekana aliingia katika mchezo kujilinda zaidi kwa kimatii tunaita Parking Bus lanzini na Antonio Michael ndo walikuwa mbele wengine wakiwa half way ya defence yao ata magoli waliyofugwa ni small error ziliwacosti ata baada ya goli walifanya vile vile
kuna mda possession ya Man city ilikuwa 82 kwa 18 ya West ham ambao kazi yao ilikuwa ni kujilinda sana Guadiola alianza na mfumo 4-3-3 Danilo akihusika kama kiungo mkabaji na kipindi cha pili alitolewa na kuingizwa Jesus aliyetoa pasi ya bao la kusawazisha aliondoa ukabaji na kuruhusu ushambuliaji Delph angecheza kama mambo yangegeuka ilikuwa ngumu maana west ham walikuwa wana goli tayari
Man city sasa mechi tatu mfululizo na 4 mashindano yote anapata ushindi dakika 10 za mwishoni alianza kwa Huddersfield ,Sauthamptom ,West ham na Uefa dhidi ya Feneyood
Uchawi uliowaumiza au kupigwa kwa hawa washika nyundo ni kutokana na kuruhusu grosi na mashuti ama pasi za boksi zinazochanganya mabeki na viungo na golikipa nataka kusema mechi izi City alizoshinda dakika za mwishoni amefunga kwa kutokana na kuruhusiwa kufanya maovu nliyoyasema De bruyne jana ndo kaua washika nyundo hawa
golikipa Adrian alifanya kazi stahiki kuokoa mashuti lakini goli la kwanza beki kijana Rice alimchanganya golikipa na goli la pili lilikuwa gumu kufuata maana mabeki walimkaba vizuri Silva na wakamuachia tena
West ham ana kazi nzito ana Chelsea ,Arsenal siku zinazokuja na zote ni derby sjui atatumia nini kuebuka ubishi huo huku city ataenda kumsalimu mourhino na kuwakaribisha Newcastle sasa Man city ameungana na vilabu vya Arsenal na Chelsea vilivyoweza kushinda mara 13 mfulilizo katika ligi kuu uingereza
Kitu kinachomfanya city kushinda magoli dakika 10 za mwishoni ni ile presha wachezaji wa timu pinzani wanamuwa nayo wanapokuwa 1-0 goli moja ni vilabu kama Chelsea na united wanalilinda Ila kwa wenzetu wanakuwa na presha sana na wanashidwa kuucheza mchezo wanaishia kuwa na presha zaidi ya kulinda suluhu ya 1-1 yaani ili umfunge city lazima ukubali ama utafute goli mbili ndo ukaze zaidi na zaidi dakika 10 za Man city ni mbaya zaidi ya dakika 80 za mchezo na kila timu ina muogopa kwa performance yake hii huwezi kukutana na city usiogope
makala na Prosper
barua pepe:barthaprosper @gmail.com
Maoni