REAL MADRID 0-3 BARCELONA.
Mchezo unaoangaliwa na mashabiki wengi duniani ulimalizika kwa timu ya nyumbani kupigwa mabao matatu sifuri.Kipindi cha kwanza Real Madrid alikuwa ameugusa mchezo akiwa amemzidi maarifa mpinzani wake Barcelona ikiwa key player alikuwa mshambuliaji Christiano Ronaldo .
Christiano akiwa na kila nafasi ya kuipatia bao Real Madrid.Huenda ubinafsi ndo ulikuwa kisu cha kuwaua Ronaldo anapata nafasi anashidwa kutoa pasi ana tafuta kufunga pasipo fungika.Katika kipindi cha kwanza klabu Barcelona walikuwa wamekubwa na presha kitu amabacho kilikuwa kigumu kwao lakini wapinzani wao Real Madrid ilishidwa kutumia mwanya huo.
Nafikiri Gerald Pique alifanya chochote kuhakikisha mipira ya vichwa haifikii wapinzani kuna mpira Gerald alikuwa hayupo kwenye boksi na Karim Benzema kupiga kichwa na kuparuza mwamba na kutoka nje ina maana klabu Barcelona ilikuwa na kazi ya kuhakikisha hawaruhusu mipira ya kichwa kuwafikia wapinzani hasa wakati viungo wa Real wanapozileta grosi kwenye eneo la hatari. na Klabu ya Madrid ilishidwa kubadilisha mbinu ya kushinda "walikaza kichwa". labda washambulie kupitia grosi za chini au kupitia kati kati waliishia kutumia mipira mirefu yaani ya juu iliyookolewa na mabeki wa katikati.
Sergio Roberto nafikiri kafanya kazi ya kufurahisha mara nyingine alicheza beki wa kati ama pembeni akiwa anabadikishana na Vermalean huku pia akienda kufanya kazi kama kiungo huku akiwa kama beki.
Mifumo ya timu zote ilikuwa 4-4-2 yaani washambuliaji wawili mbele viungo wanne wa kati wanaoweza kulinda timu zote zilikuwa zinachungulia kwa kujiami sana kwa dakika 45 za kwanza Suarez na Messi walikuwa si hatari kwa beki ya Real Madrid huku Benzema na Ronaldo wakiwa wamewasha moto wa kuwaka uliokuwa unazinwa na ulinzi wa Barcelona.
Ivan Rakitic alitembea na mpira kutoka sehemu ya ulinzi wake uwezi sema ni counter attack kwani viungo wa Madrid Casemiro na Modric "where where you " ndo labda itakuwa maneno ya Zidane kwa vijana hawa kwani alitembea free amna aliyemkaba na Roberto kufungua haraka kwa kulia na mpira kuusukuma kushoto ambapo Suarez alimaliza kazi mapema .
Nafikiri goli la Alex Vidal ni Lionel Messi kalijenga kuanzia mpira uliotoka na kurudiswa ndani na kuusukuma kwa mwenzake na kurudishiwa na baada ya kumtoka Marcelo ,Christiano hakumfuata kumkaba badala yake alimshangaa na kuona goli la Vidal likifugwa machoni mwake.
Paulinho katika mchezo wake wa kwanza wa el clasico amestabisha uma kuwa ni mtu muhimu katika kikosi cha Barcelona akifungua na kuwatoroka wachezaji wa Real madrid anakutwa sehemu ambapo timu inabaki ikistaajabu kama shuti la kwanza la Barcelona alivyoliunganisha na Navas kuutoa amekuwa kitu cha dhahabu ambacho Brazili atajivunia kuwa nacho katika kombe la dunia anakaba anafungua anafunga nafikiri alikuwa bora zaidi ya kiungo yoyote wa Real Madrid .
Marcos Ansensio pengine klabu ya Real Madrid ilikosea kumuanzisha kwani alivyochukua nafasi ya Mateo alisumbua kutafuta nafasi ya kufunga lakini ikishindikana akijaribu kwa mashuti ya mbali akijenga nafasi nzuri baadhi nafikiri angecheza na Ronaldo mwanzo wa mchezo angewafuta jasho mashabiki wa Real Madrid walioluana jasho hapa Estadio Santiago Bernabeu .
Wakati huu ata Isco na Bale hakuwaanzisha akiwatia viungo wengi walioshidwa kupika chakula nafikiri ilibidi abadilishe mfumo ili kupata nafasi ya kumchezesha Isco , Bale , Ansensio ambao wote walikuwa wakisugua benchi wakati walikuw bora sana .
Mtu kama Mateo , Modric , Casemiro walikuwa wanategeana kama goli la kwanza lilivyotokea.
kuna mpira Ronaldo kaukosa Adrea Iniesta akajitosa kuumia mpira kutoka nje akionesha mapenzi ya dhati kwa klabu hiyo kama nahodha kuhakikisha amna aibu.
Marc Ter Stegen ni moja kati ya magolikipa hatari katika dunia ya kileo alifanya ubora wake kuokoa michomo kama ya Sergio Ramos na Ronaldo , Bale ambayo ilikuwa hatari sana katika lango la upinzani.
Lionel Messi sasa kafunga magoli 15 uwanjani Santaiargo Bernabeu dhidi ya Real Madrid huku akifunga mara 10 tu dimbani Nou camp katika el clasico sasa anaongoza magoli katika Clasico akiwa amefunga mara 25 na anayemfuatia amestaafu akiwa na magoli 18 huku Ronaldo akiwa ana miaka 9 sasa katika ligi hii lakini ana magoli 8 tu katika clasico.
Ni kwa mara ya kwanza Klabu Real Madrid inapigwa mara tatu mfululizo katika laliga clasico nyumbani mfululizo 4-0 ,3-2 na leo 3-0 . Aibu inamjia raisi Fiorentina Perez.
Sasa katika ligi kuu Hispania klabu Real Madrid imepitwa alama 14 na klabu Barcelona katika laliga msimu huu ijawai tokea katika historia kukawa na tofauti hiyo na ikazibwa nafiki ni mda wa Barcelona kutwaa taji hili tena mapema tu .
Katika mechi hii Lionel Messi katoa au kaweka rekodi ya kutengeneza mabao 200 katika mashindano yote akiwa na Barcelona
Makala na Prosper Barthalomew.
simu :/ +255716243875
barua pepe :( EMAIL ) / barthaprosper@gmail.com
Maoni