UCHAMBUZI :CAF YATANGAZA WANAOSHINDANISHWA TUZO ZA MWAKA 2017,WACHEZAJI NA TIMU BORA

Shirikisho la soka barani Africa CAF  wametangaza wanaongagania tuzo za mwaka 2017.

TIMU BORA 2017 : Katika kinyanganyiro cha timu bora

Cameroon walioshinda taji la michuano ya Africa AFCON na walioshiriki michuano ya shirikisho (mabara) na kutolewa nje katika hatua za makundi walishidwa kufuzu kombe la dunia mwaka 2018.

Misri (EGYPT): ilifika hatua ya fainali na ilifanikiwa kufunzu kombe la dunia baada ya miaka 28 bila kufuzu miaka .

Nigeria :Hawakufunzu michuano ya Afcon lakini walimkunguta Argentina nyumbani kwao Argentina mabao 4 kwa 2, inaonekana ni timu itakayotoa ushindani mkubwa kombe la dunia 2018

MCHEZAJI BORA WA MWAKA :

Mohhamed Salah :Ametajwa tena katika kinyanginyiro hiki , alitunikiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017 wa BBC na ameshatia magoli 20 wavuni akiwa na jezi ya Liverpool mashindano yote huenda ikamkutia mkononi mwaka huu ukiwa unaendelea kuzama.katika ngazi ya kitaifa ameirudisha misri kombe la dunia baada ya miaka 28  na amekuwa na mchango mkubwa sana kwa taifa hilo.

Piere Emerican Abubeyang : anakipigia Dortmund ya ujerumani anahusishwa na klabu kubwa barani hapa ulaya , ameshatia magoli zaidi ya 10 ligi kuu ujerumani , katika ngazi ya kitaifa alikuwa na mchango katika kikosi cha Garbon licha ya kutofika mbali ni mshambuliaji mahiri kama nkiulizwa hilo.

Sadio Mane :Ni mtetezi katika hii tuzo anakipigia Liverpool pamoja na staa Salah napenda kuhudhuria michezo yao kwani wanacheza vizuri  .
Baada ya kutua kwa Salah  kumekuwa na tishio kubwa kwa mpinzani anayekutana  na Liverpool kwani waafrika hawa wawili ni wakali sana kwa mashambulizi.

katika ngazi ya klabu bado ana umuhimu mkubwa sana kikosini hapa .

Katika ngazi ya kitaifa aliwasaidia Senegali kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya miaka mingi na anatarajiwa kuwaongoza katika mashindano ya bara la Afrika mwanzonk mwa mwaka huu aliwafikisha mbali .

makala na Prosper Barrhalomew
simu:/+255716243875
barua pepe(EMAIL):barthaprosper@gmail.com

Maoni