TUONGEE SOKA: REAL MADRID TATIZO LA KUKUTANA NA PSG LA KWANZA HILI HAPA

Kweli hamna shabiki au ndani ya klabu ya Real Madrid ina furaha na droo ya UEFA raundi ya 16 bora.

Wamepangiwa raundi ya 16 bora na vinara wa mabao wa uefa katika makundi PSG.

Klabu ya Real Madrid watakutana na hawa moto wa jiji la Paris PSG bila kuwa na beki wa kumficha Neymar JR Dan Carvajal .

Carvajal amezuka na kuwa kati ya beki bora wa dunia kwa miaka ya karibuni UEFA wamemfungia pia mchezo mmoja wa kwanza hapo sasa Real Madrid wanakosa beki mmoja mashuuri na bora wa kuziba mabwebwe ya huyu mbrazil

Kuna Mmoroko amezuka ana miaka 19 namaana Archuf Hakimi anaweza kukaba na kuwashambulia kwani juzi Jumamosi alifunga bao safi katika mchezo wa Seville licha ya huyu kijana kuwa bora pale alipopewa nafasi wakati huyu Carvajal hakuwepo mwanzoni mwa msimu na michezo mingine

lakini tunasema Uzee dawa na maana uzoefu unamuweka mchezaji mjini licha ya Hakimu kuonesha ana kiwango bora lakini ana uzoefu pale anapokutana na mchezaji bora wa dunia kama Neymara JR ni mda mwingine wa Madrid kupata wakati mgumu wa kuziba pengo hili .

Marcelo anaendelea kukutana na kylian Mpape Mpape anakimbia nae Marcelo anakimbia sasa mchezo huu unaladha yake maalumu .

Makala Uchambuzi na Prosper Bartholomew
Simu :+255716243875
barua pepe :barthaprosper@gmail.com

Maoni