Kocha Mhispaniola Pep Guardiola anajitafutia sehemu pazuri katika ardhi ya Uingereza huenda akaitwa Sir kama ikivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson ama huenda ikamchukua muda mfupi sana kuipata heshimu hiyo ni maneno ya mdhamini tu hayana lolote tuingie katika maongezi rasmi sasa ya huyu Mhispaniola.
Alitua klabuni Manchester city msimu uliopita alimaliza msimu bila ya chochote ata cha kusafisha jina na ikawa mara ya kwanza kutokea tengia aanze kuwa kocha akiwa amepitia vilabu vya Barcelona na Bayern Munich.
Katika ligi kuu uingereza mechi 18 bila kufugwa akiwa amepata suluhu moja tu nataka nikuchambulie kama akiendelea na moto huu ataweka rekodi ngapi hatatuachia .
Kama atacheza na moto huu huenda akaipoteza rekodi ya Chelsea ya kumaliza ligi na alama nyingi kama sasa ana alama 52 katika mechi 18 Chelsea alimaliza akiwa na alama 95 msimu wa 2004-05 pamoja na msimu wa 2016-17.
Rekodi ya kushinda michezo mingi anashikilia chelsea michezo 30 alishinda msimu wa 2016-17 na sasa huyu Mhispaniola ana ameshinda mara 17 bado mara 13 na akiongeza tumsahau kama Conte alishawai kukifanya.
Kuhusu kuweka mipira wavuni ilikuwa wanaume wa Chelsea msimu wa 2009-10 mabao 103 , Pep kupata huduma ya Sane, Jesus ,Aquero ,Sterling imezaa mabao 56 yaani bado mabao 47 tu yamebakia kuwaambia wanaume wa Chelsea nao wanaweza kuwashilikia walinda mlango.
Tofauti za alama na mtu wa pili ni wanaume wa Manchester united ya nikiwa nazaliwa yaani msimu wa 1999-2000 walifanya maovu waliweka tofauti ya alama 18 wakiwa wanatwaa ubigwa lakini sasa city ana tofauti ya alama 11 dhidi ya hasimu wake yaani namba 2 anayeshikilia .
.
Chelsea walieneza ubabe msimu wa 2004 -05 sana walichukulia viwanja vya ugenini kama Stamford Bridge alisambaza vipigo 15 kwa timu za ugenini sasa City imesambaza vipigo 9 ina maana kashaanza kugeuza viwanja vya ugenini kama etihad.
Bila kupoteza sasa kinachomfanya mzee Wenger wa Arsenal kutosahulika kabisa ata akiachana na soka ni alicheza msimu mzima bila ya kupoteza mchezo msimu wa 2003 -2004 yaani huyu Mhisapaniola bado ajapoteza nae tusubirie tuone .
Sasa Manchester city imeweka rekodi ya kueleweka ya kushinda michezo 16 mfululizo .
Huyu ndo mhispaniola na kocha anayependa kazi yake na anafanya kweli mkimkenulia .
makala na mchambuzi Prosper Bartholomew
simu /+255716243875
baruapepe (EMAIL): barthaprosper@gmail.com
Maoni