klabu ya Chelsea imepanga kuandaa ofa nzito na kurudi tena Ufaransa kwa ajili ya staa huyu wa Monaco Thomas Lemar na kumtwaa staa huyu anayesakwa kwa hali na mali katika ardhi ya uingereza.
klabu za Liverpool na Arsenal zilishidwa kumsaini mchezaji huyu katika dirisha la majira ya kiangazi baada ya Monaco kukataa kwa sasa klabu ya Monaco huenda ikamwachia kwa maana wako nyuma kwa pointi tisa katika ligi na wametoka UEFA sasa wanafikiria kuwekeza katika soka la vijana ili kupata tena timu nzito kama ilivyo awali .
Chelsea huenda ikajipa moyo kwa sababu ya mkurugenzi wa soka Michael Emenelo atawapa nafasi ya kwanza kama wataenda na dau la maana na imesemekana mabigwa hawa watetezi huenda wakafungua pochi kuanzia euro 85 na kuendelea .
Kocha Antonio Conte anahitaji wachezaji kadhaa ikiwemo Philip Max wa Augsburg ya ujerumani ,Alex Sadro wa juventus .
Wakati huo huo Ross Barkley anaekaribi kupona majeraha yake Chelsea anataka kurejea kwake kwa mwendo si wakawaida baada ya kushidwa kumsajili majira ya kianagazi klabu ya Spurs inatamani sana huduma yake Ila Chelsea mda huu wana imani ya kutochezea shilingi chooni .
Makala na prosper Barthalomew.
Simu :+255716243875
barua pepe:barthaprosper@gmail.com
Maoni