Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney ameshinda tuzo ya goli bora la mwenzi novemba.
Goli alilolifunga kuikamisha hatrick yake ya kwanza baada ya siku 2,272 alipokuwa katika jezi ya Manchester united na hatrick yake ya kwanza akiwa katika jezi ya Everton .
Mpira uliokolewa na kipa Joe Hart na beki wake na goli kuwa wazi na Nahodha huyu wa zamani wa Uingereaza kufunga kwa akili kubwa kuanzia mita 58 uwanjani bado ni eneo la ulinzi la timu yake .
Mshabuliaji huyu aliyeizuru Tanzania na kucheza mchezo wake wa kwanza ameingia katika rekodi ya waliofunga magoli ya umbali mrefu akizipotezea mbali baadi ya rekodi zake pia .
Goli bora la mwenzi zawadi yake inatolewa kupitia (Carling goal of month) .
Mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji kiraka na muhimu kwani anaweza kucheza kama beki kiungo na mshambuliaji wa kati katika kikosi cha Everton chenye vijana wengi wenye umri mdogo na amekuwa kama nahodha kwa mechi nyingi za hivi karibuni hapo klabuni .
Maoni