RICARDO KAKA ASTAAFU SOKA AMETUACHIA HAYA

Mwanaume wa kukata na shoka Mbrazili Ricardo Izecson maarufu kwa jina la "KAKA" jana alitangaza uamuzi wa kuachana na soka .

Mbrazili huyu alianza soka mnamo mwaka 2001 nikiwa na umri wa mwaka mmoja tu.Yeye akiwa na umri wa miaka 18 katika klabu ya Sao Paulo kunako nyumbani kwao Brazili.

Mwaka 2003 aliwakosha sana waitalia Ac Milan na kuanza soka barani ulaya mwaka huo huku  akipata mafanikio makubwa sana klabuni hapo na kutangazwa kama mwanasoka bora wa serie A kwa miaka miwili tofauti .

Mwaka 2009 alifanya uamuzi na klabu ya Real Madrid ya Hispania ilimnasa na kupata huduma yake mpaka mwaka 2013 alipohamia kurejea Ac Milan .

Jana akiwa anatangaza kustaafu soka alikuwa anatumikia klabu ya Orlando city alicheza mchezo wake wa mwisho oktoba na uvumi ulikuwa unavuma novemba kuwa alikuwa ana tetesi ya kupewa ukurugenzi klabuni Ac milani  alizuru Ac Milan
mwenzi novemba pia

Katika ngazi ya kitaifa alivaa jezi ya Brazili mara 92 akiwa uwanjani na kupachika mabao 29 .

Akiwa Real Madrid alitwaa  copa de Rey 2009 pamoja na Laliga  2011 misimu miwili tofauti akiwa alihamia hapo kwa kuvunja rekodi ya dunia kwa wakati ule £56 Milioni .Alisumbuliwa na majeraha ya goti kabda ajachukua uamuzi wa kurudi nyumbani Ac Milani.

Akiwa Ac Milan alitwaa Serie A 2004 ,pamoja na klabu bigwa ulaya 2007 pia alitwaa tuzo ya mwanasoka  bora wa dunia mwaka huo.

Akiwa Brazilia alitwaa kombe la Dunia mwaka 2002

Ni mmoja kati ya wachezaji nane walioshinda Kombe la dunia ,la vilabu na kombe la ulaya kwa ngazi ya klabu. wakimemo wakina Zidane na wengineo

Makala na Prosper Bartholomew.
simu +255716243875.(via Whatsapp)
barua pepe (Email) : barthaprosper@gmail.com

Maoni