REAL MADRID YATWAA TAJI ,RONALDO HAZIDI KUJITANUA

Klabu ya Real Madrid inayoshiriki ligi kuu nchini hispania laliga imenyakua tena taji la kombe la dunia kwa ngazi ya klabu mara mbili mfululizo.

Katika fainali iliyopigwa dimbani Zayed sport city imeona klabu kutoka Brazili Gramio ikipigwa goli moja lilofugwa na Christiano Ronaldo kwa kutumia mkwaju wa adhabu nje ya boksi .

Huenda kukawa na minongono mingi kwani faulo ilikuwa ni kosa la refa Mmexico Cezar alivyoipuzia penati ya Gramio kutokana na rafu ya Ramos ndani ya boksi ambapo mpira ulianza haraka na kufika mguuni kwa Ronaldo aliyecheza rafu.

Katika hatua hiyo Christiano Ronaldo amefikisha idadi ya magoli 7 katika kombe la Dunia katika ngazi ya klabu akiwapiku mahasimu wake Lionel Messi mwenye 5 na luis suarez mwenye 5.

Maoni