PREVIEW WEAKEND: MASTAA KIBAO WA MOURHINO WARUDI WENGINE WAMTOSA ,PEP AJIPIGIA KIDEBE ,GUARDIOLA MBABE WA MOURHINO ZAELEZWA ,CONTE AOMBEA MABAYA HUKO MANCHESTER

JUMAMOSI 8 DECEMBA -& JUMAPILI 9 DECEMBA

WEST HAM  vc  CHELSEA;
Kipa wa west ham Adrian alifanya saves 6 katika mchezo dhidi ya City kazi itakuwa Moyes awe anampanga ama Joe Hart. Tangia David Moyes awe kocha amepata alama moja katika michezo 4 aliyosimama kama kocha. Kinachoumiza wengi west ham ina wachezaji wazuri tatizo ni nini kinachopelekea wapate matokeo mabaya?  kipindi cha Slavan Bilic Mgroatia huyu alipoiwezea West ham msimu wa 2015-16 mpaka wakashiriki Europa ligi hatua za mwanzoni alitaka mabadiliko ya mapema zaidi kipindi wanahamia London uwanjani akawanunua na kuwaleta mastaa kibaoa Antonio Michael , Adre Ayew ,Fonte,Snodgrass  , na wengineo wengi West ham hawakufanya vyema msimu uliopita akachanganyikiwa zaidi akawaleta kina Javier Hernandez na alikuwa akimtaka Kelechi Iheanacho ,akamleta Joe Hart wakati ana Adrianin kipa aliyempeleka Europa . Zaballeta yaani Slaven alitaka Revolution na amna klabu ishawai fanikiwa ivyo maana wachezaji hawa wanaitaji wamkubali mwalimu na tena walivyobadilishiwa na kuletewa Moyes asipovumiliwa mpaka February wakamfukuza tena tutawachungulia championship .

Swala la Chelsea si la kupoteza nguvu mechi saba za ligi kashinda sita na suluhu ya ugenini Chelsea anamendea alama kwa west ham na ana uhakika nazo sasa Kocha Antonio Conte kapatia mfumo wa kumtesa mpinzani 3-5-2 Fabregas kazi kubwa ni kumchungulia Morata hasa Hazard anayesipidi na ufungaji zaidi na wameshaanza ona mafanikio kisa Matic hayupo amna budi Pedro na william wawe kama super sub nyuma ya Morata na Hazard ili Kante Drinkwater na Fabregas wakabe huku moses ,(zapacosta),Alonso wawe wanafanya yote hayo Fabregas awe free mda mwingine kumchungulia kuproduce pass za kuibia za kumtesa beki mzembe ,Conte amesema Drinkwater atakuwepo pamoja na David Luiz

TOTTENHAM HOTSPURS vc STOKE CITY .
Spurs inaweza ikawa timu ya kwanza kuifunga timu moja mabao manne na zaidi katika mechi nne mtawalio. Kocha wa Stoke city Mark Hughes kathibitisha ya kuwa watamkosa Cameroon kutokana na maumivu pia mshambuliaji  Jese Rodriguez ana matatizo ya kifamilia atakosa mchezo huo .

NEWCASTLE UNITED vc LEICESTER CITY: Claud Puel anatarajia kushinda mchezo wa tatu mtawalia kwa mara ya kwanza katika ligi kuu uingereza  ,Kocha Claude Puel amethibitisha kuwakosa nyota wake Matty James pamoja na Robert Huth katika mechi ya ugenini  dhidi ya Newcastle licha ya mchezo wa kesho klabu ya Newcastle inafanya maadhimisho ya miaka 125 tangu klabu ianzishwe

LIVERPOOL vc EVERTON .Liverpool wanaweza wakaifikia rekodi yao tena ya kutofugwa na  Everton katika michezo 15 endapo watashinda mchezo wa jumapili , Jagielka  na Keane  wanatarajia kurudi katika mchezo huu. Huu  utakuwa mchezo wa kwanza watani wa jadi wa  Big Sam kama kocha wa Everton Mara ya mwisho kwa Everton kushinda Anfield ilikuwa mwaka 1999

MANCHESTER UNITED vc MANCHESTER CITY

Man city anahitaji ushindi kuweka rekodi ya ushindi wa mechi 14 mfululizo kuipoteza mbali rekodi za mechi 13 za klabu ya Arsenal na Chelsea licha yake nae ana mechi 13
Jose Mourhino na Pep Guardiola wote wameajiriwa msimu mmoja wamekutana kuanzia siku nyingi Jose Mourhino amempiga Mara 4 Pep na wametoa suluhu 6 na Mzee wa kipara Pep amepata ushindi mara 9 alipokutana na Jose

Mechi inayocheza kesho ni mechi ya 53 ya ligi kuu uingereza kwa makocha wote  timu ya José imefunga magoli 89 na kuruhusu 38 na wamepata alama 104 na timu ya Pep imefunga goli 129 kufugwa 49 na wamepata alama 121 .

Jose mourhino ameshinda michezo 29 kusuluhu mara 17 na kupoteza mara 7 na pep ameshinda michezo 37 kusuluhu 10 na kupoteza 6

Pep amesema kwamba ana uhakika wa kuwatumia David Silva na sterling anataji muda mrefu kupandisha kiwango ili acheze muda mrefu pia amesema si vizuri kucheza kufikiria rekodi inabidi ucheze kuhakikisha unashinda mchezo

Jose Mourhino amesema kwamba Phil Jones ,Zlatan Ibrahimovic ,Nemanja Matic watakuwepo na Maroune Fellaini itathibitishwa kesho ,Michael Carrick na Eric Bailly hawataikabili Manchester city

REAL MADRID vc SEVILLA
Klabu hizi mbili zina alama sawa katika ligi kuu nchini hispania atakayepata alama atajitanua zaidi  na kushika nafasi nzuri katika ligi na kumpita mwenzake kwa alama tatu  huku atakayeshinda endapo Atletico atapoteza ni nafasi nzuri ya klabu mojawapo kuwa nafasi ya tatu,Matokeo ya Real Madrid katika laliga yanatia hofu sio ya kuamini kama ilivyo msimu uliopita mechi ya juzi kule San memes wamepata suluhu ya 0-0 dhidi ya Athletic Bilbao ,Sasa timu hizi zote alama 28 nani atakuwa bora mpaka Malaga alimtesa Madrid mpaka Madrid alipopata ushindi wa bao 3-2.

ALAVES VC LAS PALMAS: huu ni mchezo wa nani anayetaka kutoka kwenye sehemu ya kushuka daraja ushindi wa Alvaves juzi jumatatu uliwatoa kutoka namba ya mwisho mpaka nafasi ya 19 endapo watashinda watapata alama 12 ambapo itategemea na ushindi wakipata ushindi wa mabao matatu watamteremsha Deportivo la Coruna ili watoke nafasi nyekundu za chini timu zote mbili zinaitaji zishinde ili kujiokoa mchezo huu utapigwa mapema mno mchana siku ya Jumamosi si wa kukosa kwani utakuwa na hamsha hamsha nyingi

VILLARREAL vc BARCELONA . Barcelona imejitanua kwenye nafasi za juu za ligi kwani ana alama 36 ajapigwa na timu yoyote katika mashindano yoyote michezo miwili ya mwisho amepata suluhu na Valencia kupata suluhu na kichapo ugenini kutoka kwa Getafe.Villarreal ina alama 21 kwenye ligi nafasi ya 6 kwenye ligi .Barcelona bado bado ijaonja uchungu wa kupoteza mchezo msimu huu katika mashindano yote .

SOUTHAMPTON vc ARSENAL . Southampton  mchezo wa mwisho wakiwa nyumbani dhidi ya Everton walisambaza kichapo cha bao 4 kwa moja ,Arsenal baada ya kupoteza kwa Manchester united na kushinda kwenye mechi ya europa kwa idadi ya mabao 6 kwa sifuri watataka kuendeleza ubabe huo kwenye ligi

Maoni