PREVIEW WEAKEND: MAJASHO KUWATOKA MAKOCHA WOTE WIKIENDI HII !

Katika ligi kuu uingereza kuanzia namba 11 mpaka 20 ukipoteza mchezo wa kesho utaanza kusaga meno ukianza kukimbia kushuka daraja vita ni Kali wa 11 ana alama 18 na wa mwisho 12.

Katika kusaka tiketi ulaya si salama na wewe ukicheka meno kesho huku kuanzia nafasi ya nne mpaka ya saba wakiwa wamelingana alama

Katika vita ya ubigwa ni wa tatu ila wapo kivuli kikubwa wamepitwa alama 11,14 respectively na Man city ya Guardiola.

Tuangalie baadhi ya michezo moto moto barani ulaya kesho

LEICESTER vc  CRYSTAL PALACE

Leicester city wameshinda michezo minne mfululizo na kutopoteza katika michezo mitano ya hivi karibuni.

Amepata alama 13 katika michezo mitano ya hivi karibuni chini ya kocha Claude Puel.

Ryard Mahrez amefunga mara tatu na kupika moja katika michezo minne ya hivi karibuni .

Shinji Okazaki amefunga mara tatu katika michezo miwili ya mwisho.

ARSENAL vc NEWCASTLE UTD.

Arsenal inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu uingereza mara ya mwisho kwa Arsenal kushinda ilikuwa mwenzi wa 11 bado wajaaonja raha ya ushinda mwenzi wa 12 .

Arsenal imepoteza mchezo mmoja na kupata suluhu 2 katika michezo mitatu ya hivi karibuni.

Newcastle bado ni wale wale kwani katika michezo saba ya ligi kuu uingereza kapoteza michezo sita na kupata suluhu moja .

Anaitaji ushindi wa lazima kuokoka kutoingia katika msitari wa kushuka daraja kwani ana tofauti ya alama 1 tu.

Kocha Rafa Benitez ana wakati mgumu na kikosi hicho kinachotumia uwanja wa mtakatifu James.

Jonjo Shevley ameoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa juzi katikati ya wiki kwa hiyo ataukosa mchezo wa Arsenal jumamosi nipigo tena kwa united.

Walijitahidi kufanya vizuri ata goli walilofugwa ilikuwa ni error ya Darlow golini kwenye ushambuliaji walijitahidi kufanya mengi sana wakigonga miamba na kutafuta chance .

kikosi cha Arsenal katika ( joto la leo ) Jana namaanisha niliwaelezea matatizo yanayowasibu kikosini. Wilshere karudi tusubirie atawapa nini klabu hii.

Tatizo la Arsenal kuna wachezaji kivuli wengi Arsene Wenger hataki kuwa muwazi kwa timu yake.

MANCHESTER CITY vc TOTTENHAM HOTSPUR'S

Klabu ya Manchester city imeshinda mara 15 mfululizo na kuweka rekodi katika ardhi hii ya Uingereza .

Inatarajia kuongeza zaidi rekodi hiyo dimbani etihad itakapowakaribisha Spurs .

Kocha bora wa mwenzi kwa mara tatu mfululizo akiifikia rekodi ya Antonio Conte wa Chelsea anatarajia kupanua wigo la alama dhidi ya mahasimu wake wanaomchungulia kwa alama 11 ,14 respectively.

Klabu ya Spurs zi nzuri sana ikiwa ugenini kwani michezo miwili ya mwisho ugenini wamepata alama 1 tu.

katika michezo mitatu ya mwisho wamefunga magoli 8 na kuruhusu mawili .
kwa upande wa city michezo mitatu ya mwisho wamefunga magoli 8 na kuruhusu mawili yaani hapo mtoto hatumwi dukani .

Msimu uliopita walivyokutana hapo dimbani Etihad walitoa suluhu ya bila kufungana .

WEST BROM vc MANCHESTER UNITED.

Tengia Alarn Perdew awe kocha wa West brim katika michezo mitatu amepata alama mbili tu na bado timu yake ijafunga goli lolote na ikiwa imefugwa goli moja tu katika ligi kuu uingerea.

Romelu Lukaku anawafunga nje ya top 6 tu klabu kama hii ijilinde na mshambuliaji huyu aliyenaswa kwa dau la pauni milioni 75. Kuanzia msimu wa 2016-17 kafunga goli 30 katika michezo 38 aliyocheza yote nje ya top 6

Mchezo wa mwisho hapa Hawathorns United alishinda kwa mabao mawili kwa sifuri yaliyofugwa na Zaltan Ibrahimovic

Utakuwa mchezo wa mwisho kwa Kiungo Paul Pogba kuukosa baada ya kadi nyekundu aliyooneshwa katika mchezo dhidi ya Arsenal.

BOURNEMOUTH vc LIVERPOOL

katika mchezo wa mwisho uliokutanisha klabu hizi msimu uliopita kulikuwa majanga kwa liverpool mchezo wa kwanza ulioalika timu yao dimbani Vitality Bournemouth alikuwa nyuma kwa bao 3 kwa 1 na kupindua matokeo na kushinda mabao 4 kwa 3, mchezo wa marudiano dimbani Anfield mambo yalibadilika na kupata suluhu .

Liverpool michezo miwili ya mwisho amepata suluhu mbili na Bournemouth michezo miwili ya mwisho kapata suluhu na kupoteza mmoja

Vijana wa mwambao wa kusini mwa uingereza wana kazi kubwa ya kuziba mashambulizi makali ya Mohhamed Salah aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwenzi na anaongoza kwa kuwa na magoli mengi katika ligi msimu huu.

A.MADRID    vc  D.   ALAVES

kuanzia msimu uliopita  Oblack ameweka clean sheat  24 akiwa amelingana na David De gea wa Manchester united anatarajia kuitukia klabu yake dimbani wanda metropolinto dhidi ya Alaves

Alaves tengia wamlete kocha mpya klabuni hapo wameshinda michezo yote miwili aliyowaongoza kama kocha .

Dhidi ya Girona walitoka nyuma na kushinda 3 kwa 2. na ushindi dhidi ya las palmas kwa mabao mawili kwa sifuri

Katika michezo miwili ya mwisho klabu ya Atletico imeshinda yote  na Deportivo nao wamefanya hivyo , dhidi ya Real Socieded walishinda mabao 2 kwa moja na juzi dhidi ya Real Betis 1 kwa 0

BARCELONA vc   RC.  DEPORTIVO

Bado ijaonja uchungu wa kufugwa klabu hii ya Cataluna inacheza mchezo kabda ya el clasico wikiendi inayokuja klabu hii wikiendi hii itacheza dhidi ya Klabu kutokea Madrid kabda ya kwenda Madrid wiki ijayo yaani kumtafuta Real Madrid .

Barcelona huenda akapata ushindi mnono kwani katika uwanja wa nyumbani imedondosha alama mbili tu tena mechi ya mwisho walipata suluhu ya bao 2 kwa 2 dhidi ya Celta de Vigo
Mechi zote za mashindano yote waliyocheza hapo wameshinda

Deportivo ana nafasi finyu ya kuzuia upenyo mkali wa timu hii dimbani Camp nou

Makala na Prosper Bartholomew
simu/+255716243875.
Barua pepe:barthaprosper@gmail.com.

Maoni