PHILIPHE COUNTINHO AMWAGA CHECHE KALI

Kiungo wa Liverpool na Mbrazil Philiphe Countinho amefunguka na kusema alikuwa anatamani kujiunga na klabu ya Barcelona katika dirisha la majira ya kiangazi

"kitakachotokea januari , tutakijua januari ,sifikiri kama kutakuwa na ofa " kiungo huyo aliongea "sifahamu maisha yangu ya soka yatakuwaje ,alisema Mbrazili huyu

Liverpool walisema Countinho si wa kuuzwa na walikataa ofa tatu kubwa za kumsajili ikiwa pauni 72 M,90 M na 114milioni

Countinho alisema katika mechi 13 alizocheza msimu huu amefunga magoli 9 .licha ya mwanzo wa msimu kuwa na majeruhi .Mchezo dhidi ya Spartak Moscow alipachika magoli matatu hatrick akiwa kama nahodha katika mchezo wa Jana usiku

Maoni