Kuhusu suala la mchezaji wa Kimataifa wa Brazil na klabu ya Livepool Phillipe Coutinho kwenda Barcelona linaonekana kukamilika baada ya Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike kuvujisha taarifa.
Nike kupitia tovuti yao waliweka picha ya jezi ya Barcelona ya msimu huu yenye jina la Coutinho, huku wakiambatanisha na ujumbe unaoonyesha kuwa nyota huyo anatua Cam Nou kabla ya msimu kumalizika.
“Philippe Coutinho yuko tayari kuipamba Camp Nou”, Waliandika Nike ujumbe huo kwenye picha ya jezi za FC Barcelona za msimu huu 2017-2018 iliyoandikwa jina la Coutinho.
makala na Prosper Bartholomew
simu :/+255716243875.
barua pepe (Email) : barthaprosper@gmail.com
Maoni