MSIMAMO:RONALDO KAWAPIGA CHINI MESSI NA SUAREZ KWA MPIGO SASA NA KUANDIKA TENA REKODI KUBWA

Mshambuliaji hatari raia wa Ureno Christiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote wa kombe la dunia kwa ngazi ya klabu baada ya kufunga goli la kusawazisha dakika ya 54.

Kabda ya mchezo wa leo jioni ina maana alikuwa amelingana na hawa washambuliaji Lionel Messi na Luis Suarez kwa magoli matano kila mmoja.

Ronaldo katika mchezo wa leo dhidi ya Al Jazira ya hapa UAE alijitahidi kuwa na nafasi nyingi za kufunga na jitihada golini na kukataliwa na Ali khasif kabda ajapata majeraha na kuingizwa kipa aliyemfunga goli Khaled Al Senani . Mchezo uliopigwa uwanjani Zayed sport City . Pasi ya bao la Ronaldo lilitoka kwa Luca Modric

Sasa Ronaldo ana magoli 6 katika mashindano haya ya kombe la dunia kwa ngazi ya klabu katika historia ni mfungaji bora wa muda wote ana mchezo mmoja wa fainali na nafasi ya kuongeza idadi ya magoli zaidi .

makala na Prosper Bartholomew
simu +255716243875
barua pepe:barthaprosper@gmail.com

Maoni