MISIMAMO: WAYNE ROONEY KIBOKO WA LIVERPOOL ,LEO MESSI KAFIKIA REKODI ,MAN CITY KAPAA

Baada ya kufunga goli moja dhidi ya Villarreal  Mshambuliaji Lionel Messi sasa ameifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich ya kuwa na magoli 525 katika timu moja aliyokuwa anayo Gerd Muller .

Wayne Rooney amekuwa nahodha kwa mara ya kwanza katika Merseyside derby na amefunga goli la kwanza katika timu hizo maana hajawai kufunga goli dhidi ya Liverpool akiwa na Everton.

Pia huyu nahodha wa zamani wa Manchester united amefunga mara tano katika mechi sita za ligi kuu uingereza alizoanza dhidi ya Liverpool .
 
Klabu ya Manchester city baada ya ushindi dhidi ya mahasimu wao Manchester united sasa wameweka rekodi ya kushinda michezo 14 mfululizo pamoja na hayo waligusa katika 18 ya Manchester united mara 40 na united waligusa mara 10. Msimu huu katika michezo 16 waliyocheza wana suluhu 1 ,ushindi 15 na kupoteza ni 0.

makala na prosper Bartholomew (mchambuzi wa Soka)
barua Pepe: barthaprosper@gmail.com
Simu:+255716243875

Maoni