MESSI ,RONALDO ,CAVANI , LEWANDOSKI KIVULINI MWA MUINGEREZA

Harry Kane mshambuliaji wa Tottenham Hotspur's ameweka rekodi mbalimbali katika mchezo wake wa mwisho wa mwaka 2017 dhidi ya Southampton katika ushindi wa bao 5-2.

Katika michuano ya klabu mwaka 2017 aliyefunga hatrick nyingi huwezi sahau kutaja jina Hary Kane
Hii ni orodha ya waliofunga hatrick mwaka 2017:-
1:HARY KANE -8 .
2:LIONEL MESSI-2.
3:CRISTIANO RONALDO -2.
4: EDERSON CAVANI -2.
6:ROBERT LEWANDOSKI -2.

Katika ligi kuu uingereza Hary Kane kwanza na miaka 24 kaonesha anaweza akazipoteza rekodi za Alarn Shealer. Rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Alarn ya kufunga magoli mengi kwa mwaka mmoja katika ligi kuu uingereza magoli 36 ya mwaka 1995 kaipoteza na kuongeza zaidi na kuwa magoli 39 kwa mwaka katika ligi ikiwa bado moja kuifikia ya Lionel Messi katika laliga mwaka 2017. kwa sasa Kane ana goli 97 katika ligi kuu uingereza akikaa kwa miaka 7 -6 inaonesha dhairi vitabu vya rekodi vitachafuliwa na jina lake.

Katika ligi kubwa tano barani Ulaya huyu kijana anayeonekana kama mrithi rasmi wa Jimmy Greaves aliyefungia klabu ya Spurs magoli 266 mwaka 1961-70 .  kwa mwaka 2017 kafunga magoli zaidi ya mchezaji yoyote barani Ulaya .

Orodha ya wafungaji mwaka 2017 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa:
1: Hary Kane -56.
2: Leo Messi -54.
3:Christiano Ronaldo -53.

Nafikiri ndo mshambuliaji wa kati barani ulaya kwa sasa kwani magoli 39 aliyoyafunga mwaka 2017 amecheza idadi ndogo ya michezo michezo 36 tu . huku hatrick 6 akifunga wakati huo wa mwaka 2017.

makala na Prosper Bartholomew.
simu:/+255716243875
barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni