JOTO LA LEO:MASHABIKI WA ARSENAL WANAVYOZIDI KUJITAFUTIA MAGONJWA ,LACAZETTE AMWAGA UKWELI KWA WAPENZI HAO
klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu uingereza mara ya mwisho kutwaa taji la ligi ilikuwa na miaka 4 yaani 2004.
Klabu hiyo imebakia ikiokota makombe mengine kama FA emirates, ngao ya hisani na kombe la ligi .
Katika ngazi ya Ulaya namanisha mashindano ya Ulaya inafurahia tu kushiriki na maana wakifika raundi ya 16 wanaogeshwa magoli mengi na kutoka .
Hawana kombe la UCL wala UEL
walifika fainali na Barcelona katika Century 21 na walipata kipigo yaani walichezea
Mashabiki huwa ni watu wavumilivu kwenye klabu hii waliandamana mpaka msimu uliopita Wenger asipate mkataba mpya lakini walitolewa nje kama wanatongoza waliandika mabango mengi ili aondoke yote yalionekana kama mapambo katika uwanja wa emirates.
Wakiwa katika mchezo wa ligi msimu uliopita katika hatua za mwishoni ilibidi shabiki apite na ndege yenye bendera imeandikwa (Wenger out) juu ya uwanja bet 365 dhidi ya stoke city .
Niwachovu wa huyu mfaransa ikafika kipindi nkaona kama wachezaji wa Arsenal wameanza mgomo maana vipigo vilikuwa vya mbwa mwitu
Msimu uliopita Chelsea alijitanua zaidi ya alama 13 jamaa akafunga macho akasema ana imani ya kucukua ligi na ata top 4 alitemwa nje .
Akapewa mkataba mnono tena wa miaka miwili yaani sasa ivi kama ujui we shabiki wa Arsenal jamaa msimu ujao tupo nae tena yaani joto linazidi kupanda .
Lacazette alinukiwa akisema Arsenal kama inataka kushinda ligi msimu huu inaitaji muujiza .
kwanza si kosa la babu yangu mzaa babu Wenger hapo hatujapoa kuhusu mustakabadhi wa Sanchez na Ozil wanaondoka bure majira ya joto .
Burnley kasimama namba sita ina tafuta tiketi ya Ulaya Spurs inajitafutia msosi nayo ulaya tena UEFA
Yaani kuanzia namba nne mpaka namba 7 ambapo klabu yetu pedwa ya Arsenal imesimama zina alama 31 na Arsenal 30 Leicester inakuja ina alama 26 ujue jinsi mambo yataamka huku Watford ana 22 na Everton ya Rooney ikiwa inakuja kwa spidi nayo 22 natamani lipicha lianze hapo Januari ndo tutamjua Arsenal Wenger ana miaka mingapi .
Mashabiki wa Arsenal wamepata alama 2 katika michezo mitatu ya hivi karibuni .
Swali langu la joto la leo kwa mashabiki wa Arsenal / Je bado mna moyo wa kutwaa ligi wakati straika gali kwenu kashakata tamaa ?
Makala na Prosper Bartholomew
simu /+255716243875
barua pepe: barthaprosper@gmail.com
Maoni