JOTO LA LEO: MASHABIKI WA LIVERPOOL WALIVYOBAKI WANAZEEKA TU ! WANAOTA MAFANIKIO

Klabu ya Liverpool inapatikana jijini Liverpool uingereza inatumia uwanja wa Anfield kama uwanja wa nyumbani

Ni moja ya klabu kubwa za kuvutia na historia kubwa ndani ya ardhi ya waliokoloni Tanzania.

Ni mji kikogwe nchini uingereza, wenye hadhi yake ya kihistoria kubwa

Turejee uwanjani tuichambue hii klabu na mashabiki wake

Tangia mwaka 1992 ambapo mfumo wa ligi kuu uingerezwa ukibadilishwa haijawai kuchukua taji hilo wakati mpaka klabu ya Leicester city inashinda taji hilo klabu hiyo ilikuwa ikihaha

Inamakombe matatu ya UCL na jumla ya makombe matano ya UEFA wakiwa waliwapa raha kubwa sana Istanbul baada ya kushinda UCL licha ya walikuwa nyuma kwa mabao matatu.

Klabu hii kizazi kipya cha mashabiki kinazidi kusubiria ligi kuu ya mfumo mpya kwani ligi kuu ile ya zamani mpaka 1992 walitwaa mataji 18 ya ligi hiyo .

Kilichowaua sana ni baada ya kuanza msimu uliopita mpaka wakaona wanachukua ligi na mwishowe kuishia kuwa wa nne mashabiki wanazidi kuumwa njaa.

klabu kama ya Everton juzi kati ilipata suluhu ya uzembe wa kocha wa Liverpool alizarau Everton akawapangia kikosi cha ajabu baada ta kushinda 1-0 alifanya mageuzi na kumtoa mwanariadha mcheaji mpira Mo Salah aliyewapa goli mguu wa Rooney ukafanya maajabu baada ya kutoa pasi ndefu kwa Calvert-lewin aliyesababisha penati na Rooney kufunga na Everton kujaza watu ndani wakulinda ushindi.

Juzi wamepata suluhu dhidi ya West brom na wanaenda kuwasaimia Bournemouth wikiendi hii kunako mwambao wa kusini mwa uingereza dimbani Vitality na msimu uliopiata waliwafunga kwa mara ya kwanza Liverpool na kuja kupata suluhu dimbani Anfield ,kocha wetu kipenzi Klopp asituzeeshe hivi hivi atujawai shangilia ligi kuu uingereza ya mfumo mpya wa 1992.

Ukiwa katika ligi ya mabigwa ulaya unaogopa kukutana na Liverpool si wa mchezo mchezo ata Siku hizi katika ligi kuna muafriaka Salah na Mane wana kimbia wanafunga vibaya hawana huruma lakini tatizo liko wapi wasiwatishie hawa wanaojichukulia kama uingereza ya kwao na maana Chelsea bigwa mara mbili kwa misimu mitatu ,Man Ferguson alivyoondoka nao wakaondoka wanarejea sasa man city kama Chelsea wanaonja raha ya ubigwa miaka ya 2010 na kuendelea kwa kimombo 2010's wanamiliki ligi hawa jamaa

Tuifikirie klabu hii tatizo liko wapi ! Kwa kocha ? , kwa matajiri ? au la hasha ?

Tuwape nafasi nyingine labda msimu ujao mashabiki wa Liverpool kijasho kitawatoka Burnley kaja ,Arsenal hayuko mbali ,Leicester ananusa , Spurs karejea. Chelsea united na city futa ndoto kushika zile nafasi tatu za juu bado uko tayari kufuzu uefa au unatania ?

Makala na Prosper Bartholomew
Simu/whatsapp +255716243875
barua pepe(Email) barthaprosper@gmail.com

Maoni