Kocha wa Manchester united Jose Mourihno amesema kuwa Mshambuliaji wake Romelu Lukaku anaitaji mapumziko ila hatampumzisha " ni mzuri kwangu lakini hapana ,siwezi mpumzisha" Jose akiongeza
Baada ya kuanza maisha vyema klabuni Manchester united katika michezo ya kwanza mshambuliaji Romelu Lukaku alianza kupoteza imani kwa mashabiki wekundu haswa pale alipofanya makosa ya ulinzi na katika kipigo cha 2-1 dhidi ya mahasimu wao pia dhidi ya suluhu ya 2-2 alionekana katika picha ya goli la kwanza baada ya kulinda vibaya .
Badala ya kumponda mshambuliaji huyo amekuwa akizungumzia zaidi kuhusu suala la mda mrefu aliokuwa uwanjani akiitumikia timu hiyo.
"Nabidi kuwa mwaminifu kwa Romelu " kwa mshambuliaji kucheza mechi 20 ,na dakika 90 zote ni muhimu kwangu na pamoja na kwa timu sina cha kumlaumu "alikuwa katika picha ya baadhi ya magoli tuliyofugwa karibuni , kwa mchezaji kama huyo anaitaji mapumziko "
Romelu lukaku amefunga mara 10 msimu huu ndani ya klabu yake mpya pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote nchini ubeligiji kwa idadi ya magoli 31.
Kosa si kwa Mshambuliaji bali Lukaku si bora kulinda timu kama ilivyo kwa mastraika ambao Mourihno amefanya nao kazi ata timu ya Everton alikuwa afanyi kazi hivyo Kocha Jose bado ataki kuelewa bado anajaribu kofosisha mambo kati ya mechi 6 alizocheza hivi karibuni amefunga mara 2 tu .
Lukaku amekuwa na matukio ya hatari ikiwemo alivyokuwa anaokoa mpira katika pambano la Arsenal na mpira kuelekea langoni mwake ambapo De gea aliuokoa mpira na baadaye kusababisha magoli mawili dhidi ya Man city na moja dhidi ya Burnley.
Katika mechi 19 za mwishoni alizocheza katika mashindano yote amefunga mara nne huku akijenga nafasi 23 katika ligi kuu uingereza .
Makala na Prosper Bartholomew
simu :/+255716243875.
barua pepe (Email) : barthaprosper@gmail.com.
Maoni