MAKALA:G.HIGUAIN AENDELEA KUITESA TIMU YAKE YA ZAMANI,ROMA YAWAKA PELEGRINI NAE AWEMO ,FREIBURG ,HUMBURG NGUVU NGUVU.

SERIE A:Klabu ya AS Roma imesambaza kipigo cha mabao matatu kwa moja kwenye mchezo wa ligi kuu Italia dhidi ya Spal magoli yalifugwa na Dzeko, Strootman,Pelegrini akifunga goli lake la kwanza katika klabu hiyo, Goli la kufutia machozi lilifugwa na Viviani aliyepewa penati na kukosa na shambulio la pili hakulikosa baada ya mkwaju huo wa penati. Nahodha wa Spal Philiphe alipewa kadi nyekundu baada ya dakika 10 tu za kwanza baada ya kumvuta  dzeko alyekuwa amempita na kubaki mwenyewe picha za VAR zikitumika kutoa maamuzi kwani refa alkuwa ametoa njano Ila kulihitaji uangalizi zaidi,na kuamua kutoa kadi nyekundu .

BUNDESLIGA: klabu za Freiburg na Hamburg zimevutana nguvu na kupata suluhu ya bila kufungana ,mchezo uliokuwa na hamsha hamsha nyingi nyingi mchezo huo ulichezwa dhimbani  Europa park nyumbani kwa Freiburg.

SERIE A:Mchezo uliokuwa unatikisa ligi kuu Italia kati ya Napoli dhidi ya Juventus umeishia Napoli akipoteza mchezo wake wa kwanza katika ligi hiyo, Mchezaji wa zamani wa Napoli anayekipigia Juventus Higuain alipata pasi safi kutoka kwa Muargentina mwenzake Paulo Dybala alyeiunganisha kulia na kufunga goli , Mchezo huo ulikuwa na mashambulizi mengi Ila ushindi wa goli moja wa Juventus ulidumu kwa dakika zote 90 .
Sasa Higuain ameifunga Napoli magoli matano katika mechi tano alizocheza dhidi yao. kabda ya kujiunga na Juventus alikuwa akiitumikia klabu hiyo ya ligi kuu Italia

LALIGA SANTANDER: Malaga nao baada ya kupoteza kwa mabao matatu kwa mawili wikiendi iliyopita uwanjani santiargo bernabeu sasa wamepata alama kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi imetoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya levante ,Malaga ipo kwenye hatari ya kushuka daraja na imepata alama moja na ikikuwa na alama 7 . imekusanya alama 8 kati ya michezo 14 inashika nafasi ya 18, levante nao wana alama 16 katika michezo 14 na wapo kwenye nafasi ya 12 kabda ya mechi za wikiendi hii

Maoni