Shirikisho la soka Duniani FIFA wamewapa adabu timu ya taifa ya Nigeria baada ya kumchezesha mchezaji aliyekuwa anatakiwa kutocheza baada ya kupewa kadi njano mbili kabda ya mchezo huo wa kufuzu kombe la Dunia .
Abdullah Shehu alicheza mchezo mzima dhidi ya timu ya taifa ya Algeria na walipata suluhu ya bao 1 kwa 1
Sasa Algeria wamepewa magoli matatu na alama tatu lakini haziathiri kufuzu kwa Nigeria kwani alichota alama za kutosha kujihakikishia kufuzu kwa kishindo katika michuano ya kombe la Dunia inayopogwa katika majira ya kiangazi mwaka ujao nchini Urusi
Pia chama cha soka cha Nigeria kinatakiwa kulipa dola za kimarekani 6000 kama adabu ya kutokuwa makini
makala na Prosper Bartholomew
Maoni