Kuna msemo unasema 'ngoja ngoja inaumiza matumbo ' msosi mtamu pale harufu inanukia alaf unamsubiria ndugu aise sawa na midomo ya watu inavyowaza kujua mengi yatakayojiri wiki ya nne lakini Kama kawaida yetu tujue ya wiki ya tatu alaf ijumaa tutajua ya wiki ya nne
Mechi ya kwanza ilicheza dhidi ya Bournemouth na Manchester city dimbani vitality vijana wa Eddie howe ndo walkuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Charles Daniels kutoka nje ya boksi kabda ya maoumziko through iliyomfikia Gabriel Jesus na kupachika bao lake la kwanza kwa msimu na la kusawazishi kipindi cha pili kilikua bana tubanane licha ya shuti lilogonga mwamba kutoka upande wa Bournemouth goli la Sterling la kiakili liliupa ushindi klabu ya Manchester city wa bao 2 kwa 1
Frankie de Boers bado klabu ina haa haa ifanyaje ipate kushinda uzembe uliofanywa na mabeki hakuuzimisha moto wa Tammy Abraham na Jordan ayew . Swansea ameonesha kiwango cha juu hasa hadi Tammy Abraham kapata moyo mzuri wa kushambulia licha ya kususua katika michezo iliyopita Mammoud sakho amerejea tena klabuni Crystal Palace labda atafanya yale makuu ya kuiokoa kutoshuka daraja
Huddersfield town almaarufu kama Terriers waliikaribisha Southampton uwanjani john Smith katika mchezo mkali . dalili ya kwanza pasipo Shaka ilimuendea Redmond licha ya kukosa goli labda haikuwa bahati safi kwa upande wao na mchezo huu ulkuwa na mashambuluzi yakutosha timu hizo katika wiki ya pili zote zilishinda kwa ushindi mwembamba
Newcastle unired chini ya Rafa Benitez walianza vibaya huku wakipoteza mechi zao yote miwili lakini wilipoikaribisha west ham haikuwa sawa kwani uwanjani st James park paliwaka baada ya ushindi mkali wa bao 3 kwa 0 Clark matrokovic nao walipachika mabao yao west ham bado inaanza vibaya msimu wake wa pili chini ya slaven Blillc pia anatarajiwa kucheza mchezo wao wa kwanza nyumbani dhidi ya Huddersfield wameruhusu goli 10 na kufunga mawili yaliyofugwa na mmexico Javier Hernandez
Watford bado ajapoteza mchezo wowote amepata suluhu mbili na ushindi mmoja watford alipokaribisha Brighton and hove albinion aliuzuia moto mkali ambao uliishia kugonga miamba na kupiga mashuti kijana Nathan cholobah bado anaonesha kazi inayoitajika uwanjani
Manchester united amezidi kujitanua katika kilele akisaka kwa uvumbi taji la ligi kuu uingereza ilipata shida L
Kusaka goli ukilinganisha na penati ya lukaku iliyotemwa nche Marcos rashford alivyopata nafasi hakuonesha kiwango kibovu hasa pale alipopata goli safi la kuongoza baada ya mkhtarian kutoa pasi ya mwisho shuti la jese lingard lilomshika au kumparuza felaini na kuwa goli liliipa klabu hii kogwe ushindi wake wa bao 2 kwa 0 dhidi ya foxes ambao wikiendi hii klabu ya Chelsea itawafuata
Kusaka pointi tatu muhimu pobga bado anazidi kuonesha ubora wake safi kabisa katika ligi hii ukilinganisha na msimu uliopita
Grosi safi iliyowekwa ndani ya jay Rodriguez wa west brom ila goli lilirudishwa kupitia peter croch ikawa 1-1 Kati ya west brom dhidi ya stoke city
Mechi Kati ya Liverpool na Arsenal ndo mchezo wa wiki kwani ulikuwa na raha mbali mbali grosi iliyopigwa kijana R.Firmino akiunganisha kabda ya S.Mane ajaongeza ikiwa kutokea upande wa kushoto labda inasemekana Roma alimuuza kwa bei rahisi ukilinganisha kiwango M.Salah alipowakimbiza mabeki wa Arsenal na kubaki na goli kipa na kufunga grosi ya huyu M.Salah haikuwa bure kwan D Sturridge aliunganisha kwa kichwa upande wa kushoto kitu ambacho kiliwakera baadhi ya mastaa wa Arsenal waliocheza mchezo huo akiwa Alexis Sanchez pamoja na mesult ozil arsenal Wenger bado ajapata nafasi ya kuchezesha wachezaji katika mifumo ya kileo ya kisoka yeye bado Ana utetea upiga pasi kufungua kuupeleka mpira kwa chini ndo vizuri licha ya kuangalia mafanikio zaidi
Tottenham Hotspur baada ya goli la dele alli labda wazo kuu lilikuwa kwamba laana ya Wembley ingeondoka ila mwishoni mpira uliompata mshambuliajj wa Burnley hakuwa pata au acha salama Tottenham Hotspur amefanyia marekebisho katika siku za mwisho za usajili labda Kama wale wachezaji aliowasajili watafanya jambo kuokoa timu hii kaongeza mshambuliaji Fernando lliorente, sergier Aurier je labda kuna jambo linaweza tokea makala hiii imechambuliwa na barthaprosper
Maoni